Main Menu

Monday, December 16, 2013

RAIS ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE AONYESHA NJIA KUACHIA MADARAKA

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amekitaka chama chake cha ZANU-PF kimtafute mtu atakayemrithi.

Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 89 na ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980, amewataka viongozi wa chama cha ZANU-PF waanze kufikiri mtu atakayemrthi yeye.

Rais Mugabe ambaye hakusema wazi na bayana kama hana mpango wa kuendelea kuwa madarakani amesema hayo kabla ya kufanyika mkutano mkuu wa kila mwaka wa chama tawala cha ZANU-PF.

Matamshi hayo ya Rais Mugabe yametathminiwa kwamba, ni tangazo lisilo rasmi la kiongozi huyo mkongwe barani Afrika la kutaka kung'atuka madarakani. 

Hivi karibuni Rais Mugabe alisema katika moja ya vikao vya chama kwamba, kiongozi ajaye wa ZANU-PF anapaswa kuchaguliwa na mkutano mkuu wa chama hicho.

Kwa mujibu wa redio tehran

0 comments:

Post a Comment