Main Menu

Sunday, November 24, 2013

RAGE AUNGURUMA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI, AKATAA MASWALI YA WAANDISHI.


DSC_0028 
Zifuatazo ni kauli za Ismail Aden Rage ambazo nimemnukuu akiongea na Waandishi kutokana na stori zilizochukua headlines kwa siku kadhaa kuhusu Kamati kumsimamisha kama Mwenyekiti wa Simba.


1. ‘Kwanza napenda kuipongeza kamati ya utendaji ya TFF kwa kuafiki mimi Ismail Aden Rage ndio Mwenyekiti halali wa Club hii ya Simba na nimepata barua yao jana ileile, katika katiba ya Simba kuna kitu wengi hawajui maana ya Kamati ya utendaji wanadhani ni wale watu saba… hapana!!! kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti… hamna kaimu hapo, kuna Wajumbe 7 waliochaguliwa katika mkutano halali… , Wajumbe saba wa kuchaguliwa mmoja wapo akiwa ni Mwanamke na wengine wawili wa kuteuliwa na Mwenyekiti, leo nitateua mwingine mmoja.. nimetoa mmoja’


2. ‘Kwa bahati mbaya Club ya Simba haina Makamu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti alishajiuzulu ila ina Kaimu Mwenyekiti tu ila huku kwenye katiba hatajwi, kwenye katiba ya Simba Makamu Mwenyekiti ana kazi mbili, moja kwa kuelekezwa na Mwenyekiti na pili Makamu Mwenyekiti anafanya kazi wakati Mwenyekiti hayupo’ – Aden Rage


3. ‘Joseph Itangire ni Kaimu Mwenyekiti tu niliemteua lakini hajapata uhalali wa kikatiba kwa hiyo katiba hii inaendelea kusema, mwenye mamlaka ya kuitisha kamati ya Utendaji mara nne kwa mwaka ni Mwenyekiti, nimekua muungwana tumefanya mara 12 mwaka huu.. kama Mwenyekiti hayupo, katiba inasema anakaimu hana mamlaka ya kuitisha kikao chochote kwa mujibu wa katiba kwa hiyo kikao kile kilichofanyika hakina tofauti na kikao cha harusi’


4. ‘Maamuzi yangu kama Mwenyekiti wa Simba sasa, kwa kuwa mkutano ule ulikua ni batili… jana niliandika barua kwa TFF kwamba viongozi hawa wamevunja katiba za TFF, Simba, CAF na FIFA… ukitaka kulalamika ni lazima uwe na ushahidi wa aina mbili unaokubalika ambao ni document na video casette iliyo na sura za watu na maneno yao waliyosema, wana document ambayo kwenye barua ya Malinzi amekiri anayo na imesainiwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba Joseph Itangire’


5. ‘Nimesikitika sana na maagizo ya TFF ya kunitaka niitishe mkutano na Wanachama wa Simba ndani ya siku 14, sijui wameitoa wapi kwenye katiba ya TFF na Simba, wamekwenda mbali na kuninyang’anya madaraka… wamenipa alafu wameninyang’anya alafu wamenipa na Ajenda ya mkutano, sasa wamenirudishia madaraka ya nini? mimi kama Mwenyekiti wa Simba… siitishi mkutano, nalindwa na katiba kwa hilo’


6. ‘Unaponipa amri unaninyang’anya madaraka yangu, katiba inasema kama naona itafaa nitaitisha… tuheshimu katiba, nilitegemea taarifa ya kwanza ya TFF mpya ingelaani mapinduzi ya kipuuzi yanayotokea’


7. Heshima yangu mimi ni Mbunge taifa linaelewa hivyo, nimekuta ofisi hii hakuna umeme miaka 18 pamoja na pazia za magunia, nimekuta uhuni mtupu.. wachezaji wameuzwa, Henry Joseph, Matole na wengine uliza wanachama wa Simba ilipata shilingi ngapi? leo imani inawatoka kusikia nimeuza Wachezaji wawili tu Congo DRC milioni 320 na nikaweka wazi hadharani sio kuwaambia Mke wangu na watoto wangu..


8. Leo nimetumiwa msg kutishia kuuwawa na tayari nimesharipoti Polisi, leo hii msg nimepata mtu kaniambia ‘Nisipotoka Simba ataniua’ alivyokua mpumbavu hajui hizi simu zinasajiliwa, nimecheki jina lake mpaka mtaa anaokaa pengine sasa yuko Lupango… why??? mpira ni burudani!! kuna mtu alikua Simba sasa yuko TFF anataka kuleta vurumai ndani ya TFF na Simba, kwa nini? kwa nini ununue watu? waandishi wa habari hebu tuache kuchochea, wewe Mwandishi ni nani ununuliwe? kuna Mwanamke Mwaandishi mmoja kalipwa milioni 2 ili anichafue, sijali.. ‘


9 Nimefanya Demokrasia sana na ndio inanitokea puani, nimeteua kamati… ziko kamati nyingi sana lakini sijaona Mwandishi hata mmoja anakwenda kuuliza kamati ya ufundi, Usajili ila kila mmoja ananishambulia mimi, leo sitaki maswali ya Waandishi wa habari, sasa mna hiari… kuandika au kuacha wala hamnipi tabu nyie, kuchafuliwa nimezoea’


10. Ukitaka kuwa kiongozi teka Ikulu kwanza, hapa ndio ikulu.

NA millardayo.com

0 comments:

Post a Comment