Klabu ya Manchester City inayoshiriki ligi kuu ya nchini England kupitia mkurugenzi wake imetangaza kuongeza ukubwa wa uwanja wao na kuufanya kuwa miongoni mwa viwanja vitatu vikubwa nchini humo.
Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zimesema kuwa upanuzi huo wa uwanja utatoka kuchukua watazamaji arobaini na nane elfu hadi kufikia sitini na moja elfu na mwezi ujao mmiliki wa timu hiyo anataraji kupata majibu ya kibali cha kuongeza uwanja huo.

Aidhaa taarifa hiyo imewatoa hofu mashabiki wa Machester City waliokata tiketi hadi kipindi cha zoezi hilo na upanuzi wa uwanja kwani lengo ni kuongeza kipato cha timu hiyo inayofundishwa na kocha Manueli Pellegrin.
0 comments:
Post a Comment