Main Menu

Tuesday, July 16, 2013

VETA YAINGIA VIJIJINI KUWAFUNDISHA MADEREVA BODABODA

mkurugenzi wa Veta kanda ya nyanda za juu kusini Monica Mbelle
 mkuu wa wilaya ya mufindi evarista kalalu akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya udereva katika kijiji cha ugesa wilayani humo
 Mkuu wa wilaya ya mufindi akikabidhi vyeti na leseni kwa madereva pikipiki

Kutokana na kuongezeka kwa watu wengi kumiliki vyombo vya moto hususani pikipiki bila kuwa na mafunzo ya udereva hali inayoongeza  ajali,  Veta kanda  ya nyanda za juu kusini imeanzisha mpango wa mafunzo ya udereva wa pikipiki hususani maeneo ya vijijini.

Akihitimisha mafunzo ya udereva wa pikipiki kwa madereva 22 wa kijiji cha Ugesa kata ya Ihalimba wilayani Mufindi, Mkuu wa wilaya hiyo Evarista Kalalu amesema pamoja na changamoto nyingi zilizopo ,serikali imeona umuhimu wa kupeleka mafunzo hayo maeneo ya vijijini na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo.


Kwa upande wake mkurugenzi wa Veta kanda ya nyanda za juu kusini Monica Mbelle amesema lengo la mafunzo hayo ni kusogeza huduma hiyo karibu na wananchi kutokana na kuongezeka kwa vyombo vya moto na kusababisha ongezeko la ajali.


Naye mkuu wa askari wa usalama barabarani wilaya ya Mufindi, Hanny Mohamed amewataka madereva hao kuendelea kujiendeleza kielimu ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha madereva ambao hawana leseni kujiunga na Veta kupata mafunzo.


Mafunzo hayo ni mpango mpya wa veta wa kuwafuata wananchi walipo na kuwapa mafunzo kutokana na uhitaji wao kwa lengo la kuwapunguzia gharama na muda wa kuvifuata vyuo  mijini.



0 comments:

Post a Comment