Timu ya taifa ya Marekani imetwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Amerika kaskazini baada ya kuifunga timu ya taifa ya Panama kwa goli moja kwa sifuri.
Marekani
wametwaa taji hilo maarufu kama kombe la dhahabu kwa mara ya tano na ikiwa ni
mara ya kwanza kutwaa ubingwa huo chini ya kocha raia wa mjerumani Jurgen
Klinsmann.
Jurden Klinsmann alishuhudia timu yake ikitwaa taji
hilo huku yeye akiwa jukwaani baada ya kufungiwa kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Honduras, Marekani
walijipatia goli pekee kupitia kwa
mshambuliaji Brek Shea.
Ilikuwa
fahari ya aina yake kwa kikosi cha timu ya taifa ya Marekani kutwaa taji hilo
ambapo kocha Jurden Klinsman alishuka jukwaani na kushangilia taji hilo akiwa
na wachezaji wa akiba kabla hata ya kipyenga cha mwisho hakijapulizwa.
0 comments:
Post a Comment