Rais wa taifa jipya la Sudan Kusini amewafuta kazi mawaziri wake
wote.
Rais Salva Kiir, mwezi uliopita aliwafukuza mawaziri wawili
muhimu, na kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya kashfa za ufisadi
wa mamilioni ya dola.
Agizo la rais kuhusu uamuzi wa kulifukuza baraza zima la mawaziri
lilisomwa jana jioni kwenye kituo cha televisheni ya taifa.
Tangazo hilo lilisema kuwa rais Kiir amewaachisha kazi mawaziri
wote, pamoja na makamu wake, na ameamuru katibu mkuu wa
chama tawala SPLM afanyiwe uchunguzi.
Sudan Kusini ilijitangaza
rasmi kuwa taifa huru mwezi Julai mwaka 2011.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment