Main Menu

Thursday, July 18, 2013

NELSON MANDELA AADHIMISHA MIAKA 95 YA KUZALIWA AKIWA HOSPITALI

Hali ya kiafya ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela imeboreka huku shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi akiadhimisha mwaka wa 95 wa kuzaliwa kwake akiwa hospitalini.

Taarifa ya Ofisi ya Rais wa Afrika Kusini imesema kama Madiba yuko hospitalini mjini Pretoria, lakini madaktari wake wamesema hali yake ya kiafya inaendelea kuboreka.

Madiba ni jina linalotumiwa na watu wa ukoo wa Mandela.

Shujaa Mandela alilazwa hospitalini tarehe 8 mwezi Juni akisumbuliwa na maradhi ya mapafu.

Umoja wa Mataifa umeitangaza tarehe 18 Julai kila mwaka kuwa niSiku ya Kimataifa ya Nelson Mandela’.

Katika taarifa kwa ajili ya siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema siku hii inalenga kuwahimiza wanaadamu wafanye bidii kuleta amani, usawa na maendeleo endelevu duniani.


na radio tehran

0 comments:

Post a Comment