Main Menu

Thursday, July 4, 2013

MUDA MFUPI BAADA YA MAPINDUZI, MISRI YAPATA RAIS MPYA

Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Katiba nchini Misri leo ameapishwa kuwa rais mpya wa kipindi cha mpito na kuchukuwa madaraka masaa kadhaa baada ya jeshi la nchi hiyo kumpindua Rais Mohamed Mursi. 


Jaji Adly Mansour amekula kiapo hicho katika makao makuu ya Mahakama ya Katiba yaliyoko pembezoni mwa Mto Nile mjini Cairo katika hafla iliyotangazwa hewani moja kwa moja na televisheni ya taifa. 

Kwa mujibu wa agizo la kijeshi Mansour atakuwa kiongozi wa serikali ya mpito nchini Misri hadi hapo rais mpya atakapochaguliwa. 


Tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mpya bado haikutangazwa.


Mursi ambaye alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokorasia nchini humo mwaka mmoja uliopita amekuwa kwenye kifungo cha nyumbani katika mahala ambako hakukutajwa tokea majenerali wamuondowe madarakani hapo jana katika kile wafuasi wake walichokiliaani na kukiita kuwa ni mapinduzi ya kijeshi. 


Takriban washauri na wasaidizi wake kadhaa pia wako katika kifungo cha nyumbani. 


Waendesha mashtaka wameamuru kukamatwa kwa viongozi waandamizi chama cha Udugu wa Kiislamu.

Dw swahili

0 comments:

Post a Comment