Main Menu

Monday, July 15, 2013

MABOMBA KWA AJILI YA KUSAFIRISHA GESI TOKA MTWA YAWASILI NCHINI

Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Freight Forwarder Bibi Vanessa Gwau kushoto akielezea jambo kwa mwandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabomba yatakayotumika kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadio Dar es Salaam. Jambo Freight ndiyo kampuni iliyopewa zabuni ya kupakua shehena hiyo.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu Youging katikati akifafanua jambo,kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Prosefa Sospeter Muhongo,kutoka kulia Ms Wang Fang kutota Ubalozi wa China anayemfuatia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sadick Meck Sadick.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akiwasili katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam tayari kwa kuzindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabomba yatakayotumika katika ujenzi wa mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda katika akibadishana jambo na Waziri wa Nishati na Madini Prosefa Sospeter Muhongo aliyekaa kushoto,Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lu Youging wakati wa hafla ya kuzindua kupokea shehena ya mabomba kwa ajili ya mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akishuhudia Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu Youging alipokuwa akimalizia kufunua kitamba kama ishara ya uzinduzi rasmi wa upakeaji wa mabomba ya Gesi.
Pichani mafundi wakiwa katika zoezi la kupakua mabomba kutoka katika meli na kupakia kwenye Lori tayari kwa safari ya Mtwara.
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi upokeaji wa mabomba ya gesi tayari kwa kusafishwa hadi Mtwara.
 
 PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA - MAELEZO

Serikali imewatoa hofu wananchi wa Mtwara kuhusu kunufaika kwao na gesi asilia iliyopatikana katika maeneo yao.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda alipokuwa akizindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabonba ya gezi kwa ajili ya mradi wa bomba la kusafirishia Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam mwisho ni wiki jijini Dare se Salaam.

Pinda amesema kuwa wananchi wa watanzania watanufainaka na mradi huo hasa hasa wakazi wa Mtwara kwakuwa vijana wengi watapata ajira wakati na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo kwakuwa viwanda mbalimbali vitajengwa mkoani Mtwara kikiwemo kiwanda cha Saruji ambacho ujenzi wake umekwisha anza.

“Ndugu zangu wana Mtwara ni waambe tu wakati wa kunufaina na rasilimali ya Gesi sasa umefika,niseme tu mradi huu utakapokamilika fursa mbalimbali zitafunguka ikiwemo ajira kwa wakazi wa Mtwara”. Alisema Pinda. 

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Balozi Lu Youging amesema kuwa Tanzania itanufaika na mradi huu na kukua kiuchumi kwakuwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi katika nishati na badala yake itazalisha nishati yakutosha.

Balozi huyo aliongeza kuwa kutpitia mradi huu Tanzania itaondokana na kuwa tegemezi katika shughuli zake za maendeleo kwa kuwa kuna hazina ya kutosha ya gesi asilia na itawanufaisha watanzania wenyewe na si vinginevyo.

Jumla ya mabomba 3400 yamepokelewa katika awamu ya kwanza ambapo awamu ya pili itapokelewa shehena yenye mabonmba 4600 katika bandari ya Mtwara.Inakadiriwa kuwa jumla ya shehena 12 zitatumika mpaka mradi utakapokuwa umekamilika.

0 comments:

Post a Comment