MEYA wa wilaya ya Ilala, Jerry Slaa
amewataka warembo wa wilaya ua Ilala kuangalia mbele zaidi mara baada ya
shindano hilo waone kuna vitu wamejifunza ili kuweza kuwasaidia katika maisha
yao ya baadae.
Slaa aliyasema hayo juzi alipowaalika
warembo hao katika ofisi zao kwa lengo la kuizundua rasmi kambi ya Miss Ilala
katika shindano linalotarajiwa kufanyika Agosti 16 kwenye ukumbi wa Golden
jubilee Tower uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
“Naomba muangalia baada ya mashindano
ya Miss Ilala, nini mmenufaika nacho ili kuweza kuwasaida zaidi huko mbele ya
safari, lakini vile vile kufanya kazi za kijamii na kuondoa dhana kwamba urembo
ni uhuni,” alisema Slaa.
Aliwataka warembo hao kuwa wapesi wa
kubuni na kujifunza mambo ili nao waweze kuwasaida wenzao lakini pia wao mfano
kwa wengine na kuwahamasisha njia mbalimbali za kukabiliana na maisha na
kuwajenga moyo wa kutokata tama.
Katika mkutano huo ambao warembo
walimuuliza maswali mbalimbali Meya huyo kijana mwenye upeo mkubwa wa uongozi,
ataungana na warembo hao katika kufanya kazi mbalimbali za kijamii na kujitolea
katika wilaya ya Ilala katika kipindi cha mwezi mmoja watakaokuwa kambini.
Jumla ya warembo 15 wa Kanda ya Ilala walianza mazoezi rasmi
katika ukumbi wa klabu Billicanas juzi iliyopo
katikati ya jiji la Dar es Salaam na Mkurugenzi wa WMP Promotion, William
Malecela inayoandaa shindano hilo, alisema jana kanda yake itahusisha warembo
kutoka vituo vya Tabata, Ukonga na Mzizima na Dar city centre.
Taji hilo kwa sasa linashikiliwa na
Noela Michael, mshindi wa pili ni Magdalena Munisi na mshindi wa tatu alikuwa
Mary Chizi ambao waliwakilisha kanda ya Ilala katika mashindano ya Miss
Tanzania mwaka jana.
Warembo hao watakuwa chini ya mwalimu
wao, Suzy Makassy akisaidiwa na Otelia Johnsen kutoka Norway huku Edda
Sylvester ni pamoja na Alice Issac,
Clara poul,Maria Peter, Anna Johson, Iren Mwelolo,Rehema Mpanda,Martha Gawe,
Diana Joackim, Natasha Mohamed, Dorice Mollel, Pendo Lema, Kazunde Mussa na
Kabula Kibogoti
Malecela alisema, pia kutakuwa na
jopo la wakufunzi wa dansi, litakaloongozwa na msanii Japhet aliyekuwa katika kundi la kuibua vipaji la
Tanzania House of talent (THT) yote katika kuhakikisha shoo ya mwaka huu
inaendana na ubora wa warembo wanaoshiriki shindano hilo.
Ilala imewahi kutoa warembo kadhaa
miaka ya nyuma, waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi
nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika nyanja mbalimbali za urembo na
ubunifu wa mavazi.
Miongoni mwao ni Hoyce Temu,
Jacquliney Ntuyabaliwe, Angela Damas na Salha Israel.
Shindano hilo linalotarajiwa kuwa na
burudani ya kipekee limedhaminiwa na kinywaji cha Redd’s, Dodoma Wine, magazeti
ya Jambo Leo na Tanzania Daima, Blogu ya Wananchi (Le Mutu), CXC Africa Tours & Safaris, Clouds FM,
Times FM, Delina Enterprises.
0 comments:
Post a Comment