Main Menu

Wednesday, July 24, 2013

BAADA YA KUDAIWA KUTAKA KUBAKA MTANGAZAJI WA R.F.A KUIFIKISHA MMILIKI WA BLOG ILIYOTOA TAARIFA HIYO MAHAKAMANI

HABARI mabibi na mabwana...kwa heshima na taadhima naomba nichukuwe fursa hii kuzungumza JAMBO zito kidogo...jumamosi ya wiki iliyopita tarehe 21 mida ya jioni nilipigiwa simu nyingi sana, nikatumiwa sms nyingi na inbox nyingi pia kufahamishwa jambo lililonishangaza na kuniacha nikiduwaa. Jambo lenyewe ni kuhusu HABARI ilioandikwa kwenye BLOG ambayo hapo kabla nilikuwa siifahamu kabisa (nimei'link hapa chini)...HABARI inayonihusu mimi...baada ya kuisoma HABARI hiyo niliamua kutulia kwanza na kutokusema chochote japo watu wengi walinipa ushauri wa ku'clear the air...tangu jumamosi mpk hii leo siku kadha zimepita...kuna sababu ambazo zilinifanya nikae kimya kwa muda wote huo...KWANZA nilihitaji muda wa kutafakari na PILI nilitaka mpaka nije nizungumze hapa ni lazima niwe nimeanza kuyafanyia kazi maamuzi niliyofikia...NASHUKURU hilo limefanyika.

NDUGU ZANGU...HABARI HII HAINA UKWELI HATA CHEMBE MOJA...lakini napenda niwafahamishe kuwa ni wazi kabisa kuwa nyuma ya HABARI hii kuna vitu vingi sana ambavyo sidhani kama nastahili kuvizungumza hapa coz nadhani hata mimi pia havinihusu (vitu vya kihistoria nilivyovikuta IRINGA mwaka jana nilipokwenda kufanya kazi na kituo cha redio cha EBONY FM kabla sijahamia RFA mwaka huu)...lakini nyuma ya habari hii kuna MTU (Mmiliki wa BLOG yenyewe) ambaye mpaka sasa najiuliza NIA yake hasa juu yangu mimi ni ipi...?Anataka kuona nini kikitokea kwangu...?MTU huyu SIMFAHAMU, HANIFAHAMU (labda kwa kunisikia tu), hatujawahi kuonana wala kuzungumza...sasa SIELEWI kwanini anafanya hivi...najiuliza hivi inawezekanaje mtu kumchukia mtu mwingine ilhali hamjawahi hata kuonana...?INASIKITISHA SANA...INASIKITISHA mno kuona wakati KIJANA mmoja wa kitanzania akijitahidi kutimiza NDOTO zake kuna kijana mwingine wa kitanzania anajaribu kumkwamisha na kumrudisha nyuma kwa kutumia njia ya kumchafua ili aonekane hafai mbele ya JAMII.

MARAFIKI zangu...mimi ni KIOO cha jamii na hakuna mtu atakaenielewa kama nikijaribu kufanya hicho kilichoandikwa kwenye HABARI hii...kibaya zaidi ni kwamba hata huyu aliyeamua kuandika habari hii ameiandika bila kufanya UTAFITI wa mazingira ya RFA na SAHARA MEDIA kwa ujumla...kutokana na HABARI yenyewe ni ngumu kwa TUKIO hilo kufanyika katika mazingira haya...KWANZA kabisa sisi kama watangazaji hatuna ruhusa ya kumpokea mtu getini anayetakiwa kufanya interview kwenye kipindi...tunachokifanya ni kuandaa kibali cha mgeni huyo kupita getini na kazi yetu inakuwa imeishia hapo...kazi inayobakia ni kumuona akiwa tayari ameshaletwa studio kwa ajili ya interview hiyo...sasa inaposemekana kuwa eti msanii huyo alifika getini na kunipigia simu na nikaahidi kwenda kumchukuwa ni kitu kisichowezekana na inaonesha wazi UBABAISHAJI wa mtunzi wa HABARI hiyo...PILI mgeni yeyote hasa asiye na kibali haruhusiwi kumsubiri mtangazaji getini especially USIKU...TATU...kipindi cha FRIDAY WEEKEND FEVER huwa hakitambulishi nyimbo mpya za wasanii na hakijawahi kufanya hiyo KAZI...hiyo ni KAZI ya kipindi cha SHOWTIME NEW CHAPTER ambacho huwa mchana kuanzia saa 8:00 - 10:00 jioni...NNE...katika kipindi cha FRIDAY WEEKEND FEVER nimeshafanya interview moja tu (na K-RECORDS lebelmates) na hiyo ilikuwa ni MIEZI mitatu iliyopita...sasa swali ni je TUKIO hilo limetokea MIEZI hiyo mitatu iliyopita..?(coz HABARI haijaahinisha limetokea lini)...na kama ni miezi mitatu iliyopita iweje lije lijulikane hivi sasa...? na TANO...kwa kawaida watangazaji wote tunaotoka katika vipindi vya USIKU huwa tunarudishwa nyumbani na gari ya OFISI...gari ambayo huwa tunapanda tukiwa ndani ya uzio wa eneo la kazi na geti hufunguliwa na walinzi kwa ajili ya kuruhusu gari hiyo kutoka...sasa sijui pia binti huyo tulikuwa nae katika gari hiyo kuelekea huko ambako HABARI hiyo inasema...??Ni nini...?Au ni kutafuta attantion wa WATU kwenye BLOG yake ili ipate wasomaji...?lakini mbona kuna vingi vya kuandika ili BLOG isomwe na watu wengi kama NIA ni hiyo...?kwani DJ CHOKA alifanya nini mpaka BLOG yake hivi sasa imefikisha watazamaji milioni nane...?INASHANGAZA SANA.

NDUGU zangu...binafsi sijawahi kuzungumza, kukutana wala kuonana na MSANII yeyote wa kike wa MWANZA tangu JAN nimekuja MWANZA...MIMI ni MTU safi, mwenye HESHIMA zangu, nina MTOTO wa kike ninayempenda na kumuheshimu sana...ambaye kama mimi leo nikifanya hicho kilichoandikwa kwenye BLOG hiyo what if naye akija kufanyiwa...?SIWEZI...!!Kwanza MIMI ni nani nifanye tukio kama hilo na leo niwe URAIANI..?Hii nchi haina SHERIA...??mimi ni nani katika serikali hii mpaka leo hii niwe SIJAKAMATWA...?Na kama TUKIO hilo limetokea MWANZA kwanini lisianze kujulikana MWANZA...??livuke MIKOA mpaka kwa mmiliki wa BLOG ambaye yuko IRINGA (sina HAKIKA)...Ni WAZI kabisa kuwa hii ni kampeni ya mtu (au WATU) wanaotaka kuniharibia...ni kampeni ya WATU wasiotaka kuona NIKIFANYA hiki ninachokifanya hapa...NDUGU ZANGU nina NDOTO nyingi sana ambazo HAZIJATIMIA na ninafurahi kuona kwa sasa niko sehemu ambayo nauona MWANGA...watu hawa wanataka KUNIRUDISHA NYUMA...tafadhalini TUWAKEMEE..!!ni UDHALILISHAJI.

MARAFIKI..nashukuru MUNGU kwa support niliyoipata kutoka kwa wakuu wangu wa KAZI hapa SAHARA MEDIA...hili jambo haliwezi kupita hivihivi...ni LAZIMA nichukuwe hatua...KIBAYA zaidi ameigusa na kampuni ninayofanyia kazi (SAHARA MEDIA)...SHERIA zipo na MWANASHERIA yupo pia...laa sivyo hawa watu watazoea...na kama si mimi basi kesho mwingine tena atachafuliwa...ni lazima TABIA hii ikomeshwe...naanza mimi kuikomesha TABIA hii...nimeshaanza kuchukuwa HATUA...na napenda pia nichukuwe FURSA hii kumwambia huyu mtu (Watu) kwamba atakamatwa tu...ni lazima AKAMATWE...Serikali ina MKONO mrefu...aulize yaliyomkuta mmiliki wa BLOG ya ZEUTAMU...AKHSANTENI...!!

1 comments:

B & S MPAJI NI MUNGU said...

aaahaaaa inanishangaza kuona watu wameshindwa kuandika habari za kujenga taifa na wanafanya yao yasio husu taifa hii ni hatari sana

Post a Comment