Main Menu

Sunday, May 19, 2013

WATU ZAIDI YA 50 WAKAMATWA KUTOKANA NA VURUGU KATI YA WAMACHINGA NA POLISI MKOANI IRINGA, MBUNGE WA IRINGA MJINI ASAKWA NA POLISI

GARI la  Mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji peter Msigwa akiondoka  eneo la mashine  tatu  ambapo wamachinga walikua wakifanya maandamano
  wamachinga wakisukuma gari la mbunge msigwa wakati wakifanya maandamano ambyo baadae yalitawanywa na polisi
abiria katika eneo la stand kuu manispaa ya iringa wakikabiliana na moshi wa mabomu ya kutoa machozi kwa kutumia maji
               hali ilikua hivi katika baadhi ya mitaa ya iringa





Kamanda wa polisi mkoa wa iringa SACP KAMUHANDA akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema zaidi ya watu 50 wamekamatwa wakiwemo wanawake 4.

Kamuhanda amesema hakuna madhara makubwa yaliyotokea kwa binadamu na kwa upande wa uharibifu ukubwa uliofanywa ni kwa gari la zimamoto ambalo limepasuliwa vioo na askari wake mmoja kujeruhiwa mguu.

Hata hivyo kamanda huyo ameongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kumtafuta mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa ili aunganishwe na watuhumiwa wenzake kwa kufanya maandamano bila kuwa na kibali.

Mchungaji Msigwa asubuhi ya leo aliungana na wamachinga kufanya maandamano kupinga zuio la kufanya biashara eneo la mashine tatu kwa madai kuwa eneo walilopelekwa la mlandege hakuna biashara na miundombinu haijawekwa sawa.

Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Teresia Mahongo amewataka wamachinga kufuata sheria na kuendelea kufanya biashara katika eneo la mlandege wakati malalamiko yao yanafanyiwa kazi.

Aidha kamuhanda amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani jeshi la polisi limefanikiwa kudhibiti hali ya machafuko na linaendelea na doria katika maeneo mbalimbali ya manispaa.

0 comments:

Post a Comment