Main Menu

Sunday, May 26, 2013

TAIFA STARS WATOKELEZEA NA SUTI MPYA TOKA KWA WADHAMINI WAO KILIMANJARO PREMIUM LAGER


Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania, Phocus Lasway (kulia) akikabidhi vazi la suti mpya maalum kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah wakati wa hafla maalumu ya kuonesha vazi hilo la suti mbele ya wageni mbali mbali waliohudhulia hafla hiyo,iliyofanyika jana jioni kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar. Wa pili kulia Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
Wachezaji wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wakipita jukwaani huku wakiwa wamevalia suti hizo wakati wa hafla maalum ya kuonyesha mavazi yao hayo iliyofanyika jana jioni Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar.
Wachezaji wa Taifa Stars, benchi la ufundi na maofisa wakuu wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuonesha suti mpya
Wachezaji wa Taifa Stars na benchi la ufundi katika picha ya pamoja.
Wadau wa soka nchini wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi suti mpya kwa Taifa Stars.

PICHA KWA MSAADA WA MICHUZI


0 comments:

Post a Comment