Main Menu

Sunday, May 26, 2013

AL SHABAB WAZIDI KUITESA KENYA KWA MASHAMBULIZI

Watu sita wameuawa wakiwemo askari polisi wawili baada ya wanamgambo wa kundi la al Shabab la nchini Somalia kushambulia kituo cha polisi kilichoko eneo la Liboi kaskazini mashariki mwa Kenya.

Charlton Mureithi Kamanda wa Polisi wa eneo hilo amesema kuwa, watu wenye silaha walivamia kituo hicho cha polisi na kufyatua risasi hapo jana usiku, na kusababisha maafa hayo. 

Imeelezwa kuwa mara baada ya serikali ya Kenya kutuma wanajeshi wake nchini Somalia mwaka 2011 kwa lengo la kuwatokomeza wanamgambo wa al Shabab, nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi na milipuko ya mabomu yanayofanywa na wanamgambo wa kundi la al Shabab kwenye eneo la mpaka wa Somalia na Kenya. 

Kundi la al Shabab la nchini Somalia leo limetoa taarifa na kuthibitisha kuwa ndilo lililotekeleza shambulio hilo.

0 comments:

Post a Comment