Main Menu

Monday, April 29, 2013

ZIARA YA RAIS KIKWETE MKOANI MBEYA YASOGEZWA MBELE, KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MEI MOSI TAIFA,AFUTA ZIARA YA KUTEMBELEA MIRADI MBALIMBALI MKOANI HUMO

MKUU wa Mkoa wa Mbeya ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jkaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe,kesho aprili,30 majira ya saa 4.30 asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo ,abbas Kandoro amewataka radhi kwa usumbufu wakazi wote kutokana na mabadiliko ya ratiba ya ziara ya Rais kutokana na kujitokeza dharura ya mkutano wa jumuiya ya Afrika mashariki uliofanyika mjini Arusha .

Aidha Kandoro amekanusha uvumi uliotokea  kuwa Rais ameahirisha kabisa ziara mkoani Mbeya kwamba sio kweli kwani baada ya kuwasili kesho ataelekea moja kwa moja kuzungumza na wamiliki, mameneja na wakuu wa shule za msingi, sekondari na vyuo binafsi TAMONGSCO Taifa katika ukumbi wa mkapa, sokomatola jijini Mbeya.

Mkuu wa mkoa amesema baada ya kutoka hapo Rais kikwete atapokea taarifa ya Mkoa katika ikulu ndogo na baadaye kukutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi ambapo Mei mosi atakuwa mgeni rasmi katika siku kuu ya wafanyakazi kitaifa inayofanyika katika viwanja vya sokoine, jijini Mbeya.

Aidha Kandoro amesema sherehe za mei mosi zitaanza asubuhi hadi jioni ambapo Rais Kikwete ataondoka baadae kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya shughuli nyingine za kitaifa na kwamba zile shughuli zilizopangwa kutembelewa na Rais na kufanya uzinduzi zitapangiwa  ziara nyingine itakayotangazwa hapo baadaye.

Ametaja sehemu zilizopangwa awali kabla ya kubadilisha ratiba  ni pamoja na maghala mapya ya kanda ya MSD yaliyopo Iwambi,Uwamu Saccos Uyole,,Kiwira Benki Kata,Ikama,Kiwanda cha gesi ukaa,Mradi wa maji Kamabasegelo,Iyula wilayani Mbozi na igurusi wilayani Mbarali .

0 comments:

Post a Comment