Main Menu

Friday, April 12, 2013

UJUMBE WA FIFA KUWASILI NCHINI APRILI 15


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwatangazia wadau wa mpira wa miguu kuwa ujumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utawasili nchini Jumatatu (Aprili 15 mwaka huu) kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa uchaguzi mkuu wa TFF.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, ujumbe huo utaongozwa na Mkuu wa Idara ya Uanachama ya FIFA, Primo Covarro na utafanya kazi kwa siku tatu kuanzia siku ya ujio na kuondoka Aprili 18 mwaka huu.

Ukiwa nchini, ujumbe huo utakutana na wagombea uongozi walioathiriwa na uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambao waliomba mashauri yao yaangaliwe upya, wagombea ambao walikata rufani FIFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya Rufani na Sekretarieti ya TFF.

Wajumbe hao wangependa kukutana na waziri anayehusika na michezo, hivyo TFF imeiandikia Wizara ikipendekeza kuwa ujumbe huo ukutane na Waziri na wakuu wengine wa michezo Aprili 16 mwaka huu 2013 kabla ya kuanza kazi zao.

Wagombea watakaosikilizwa na ujumbe huo wa FIFA ni:
1.   Farid Salim Mbaraka Nahdi: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alienguliwa na Kamati ya Uchaguzi na baadaye rufani yake kwa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kutupwa na hali kadhalika ombi lake la kutaka shauri lake liangaliwe upya, kukataliwa.

2.   Elliud Peter Mvella: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na kukata rufani Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF kabla ya maombi yake ya kutaka shauri lake kuangaliwa upya, kukataliwa.


3.   Mbasha Matutu: Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi na kukata rufani ambayo pia ilitupwa kabla ya kuomba shauri lake liangaliwe upya, ombi ambalo lilikataliwa.

4.   Hamad Yahya: Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ligi ambaye alipitishwa na Kamati ya Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na kuondolewa. Aliomba shauri lake liangaliwe upya, lakini Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ikatupa ombi lake.

5.   Jamal Emily Malinzi: Mgombea wa nafasi ya urais wa TFF ambaye alipitishwa na Kamati ya Uchaguzi, lakini mwekaji pingamizi akakata rufani ambayo ilikubaliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, hivyo kuondolewa kwenye mchakato. Aliomba shauri lake liangaliwe upya, lakini likakataliwa. Hata hivyo, alikuwa ameshakata rufani FIFA.

6.   Michael Wambura: Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF ambaye alikatwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na rufani yake kukataliwa na Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF. Hakuomba shauri lake liangaliwe upya, lakini alikata rufani FIFA.

Shirikisho linawaomba wote waliotajwa hapo juu kujiandaa kwa utetezi na maelezo ya kutosha na kwamba barua za kuwaita zinafuata. 


TFF GENERAL ELECTIONS

ORODHA YA WALIOATHIRIWA NA MAAMUZI YA KAMATI YA RUFAA


NA.
JINA
NAFASI ALIYOGOMBEA
UAMUZI WA KAMATI YA UCHAGUZI
UAMUZI WA KAMATI YA RUFAA ZA UCHAGUZI
OMBI LA SHAURI KUANGALIWA UPYA AU UAMUZI WA KUKATA RUFAA FIFA
1.
Ahmedi Yahaya
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu
Aloipitishwa
Aliondolewa
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
2.
Mbasha Matutu
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu)
Aliondolewa
Aliondolewa
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
3.
Farid Salim Mbaraka Nahdi
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF (Morogoro na Pwani)
Aliondolewa
Aliondolewa
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
4.
Eliud Peter Mvella
Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Iringa na Mbeya)
Aliondolewa
Aliondolewa
Aliomba shauri lake liangaliwe upya
5.
Jamal Emily Malinzi
Urais wa TFF
Alipitishwa
Aliondolewad
Aliomba shauri lake liangaliwe upya na alikata rufaa FIFA
6.
Michael Richard Wambura
Makamu wa Rais wa TFF
Aliondolewa
Aliondolewa
Alikata rufaa FIFA


PROGRAMU YA UJUMBE WA FIFA NCHINI

PROGRAMU YA SIKU TATU (Tarehe 15 – 18 Aprili 2013)



Date / Time

Activity
15 Aprili 2013
Saa 12:30 – 03:00
Kuwasili kwa wajumbe wa FIFA
15 Aprili 2013
Saa 04:00 – saa 05:00 usiku
Kikao na Rais wa TFF pamoja na Sekretarieti
16 Aprili 2013
Saa 04:00 – 05:00 asubuhi
Kwenda ofisini kwa Waziri wa Michezo kwa ajili ya kumsalimu
16 Aprili 2013
Saa 05:30 – 06:30 asubuhi
Kukutana na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupata taarifa ya uchaguzi
16 Aprili 2013
Saa 06:30 – 08:00 mchana
Chakula cha Mchana
16 Aprili 2013
Saa 08:00 – 12:00 jioni
Kukutana na wagombea walioondolewa
17Aprili 2013
Saa 03:00 – 05:00 asubuhi
Kukutana na Kamati ya Rufa za Uchaguzi ya TFF
17 Aprili 2013
Saa 05:30 – 06:30
Mchana
Kupewa taarifa zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi, i.e., kesi zilizo mahakamani

17 Aprili 2013
Saa 08:00 – 10:00 jioni
Kukutana na watu wengine ambao FIFA wanaweza kuomba kukutana nao
17Aprili 2013
Saa 10:30 – 11:00 jioni
Mkutano na waandishi wa habari – kushukuru mamlaka na pande zilizohusika kwa ushirikiano
18 Aprili 2013
Saa 10:00 – 12:00 Alfajiri
Kuondoka hotelini kwa ajili ya safari
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

0 comments:

Post a Comment