Main Menu

Sunday, April 7, 2013

KOREA KASKAZINI YAJIANDAA KUFANYA JARIBIO LA NYUKLIA


Mkurugenzi  wa usalama wa taifa wa Korea Kusini, amesema Korea Kaskazini inaweza ikawa inaandaa jaribio la nyuklia au kufanya kitendo kingine cha uchokozi, kwa kutoa tahadhari ya kutohakikisha usalama wa wanadiplomasia. 

Onyo hilo la wiki iliyopita la Korea Kaskazini linafuatia vitisho vya vita vya wiki kadhaa na jitihada za kuiadhibu Korea Kusini na Marekani kutokana na mazoezi ya kijeshi ya pamoja yanayoendelea, pamoja na hatua ya nchi hizo mbili kuunga mkono vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi yake. 
 

Alhamisi iliyopita, waziri wa ulinzi wa Korea Kusini, alisema Korea Kaskazini imehamishia kombora lake la masafa marefu katika pwani ya mashariki na kuna uwezekano wa kufanya jaribio la nyuklia. 

Amesema kombora hilo linaweza kuwa aina ya Musudan, lenye uwezo wa kushambulia kambi za Marekani zilizoko Guam na inakadiriwa kuwa lina uwezo wa kuruka hadi kilomita 4,000.

0 comments:

Post a Comment