katibu mkuu wa chadema dr wilbrod slaa akizungumza na wanachini wa mji wa iringa katika mkutano uliofanyika leo katika viwanja vya mwembetogwa mjini humo
dr slaa akifafanua jambo
umati mkubwa wa wanachama na wakazi wa mji wa iringa na viunga vyake
mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akikunja ngumi kwa ajili ya people powerrrr
PEOPLEEEEEEEEEEEEEEEEEE.........POWER!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Ni takribani wabunge watano waliotolewa bungeni kwa kile kinachodaiwa utovu wa nidhani wakiwa na katibu mkuu wa chama hicho Dr Wilbrod slaa wapo ziarani katika baadhi ya mikoa kwa kile walichodai kumshtaki spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Anne Makinda na naibu wake Job Ndugai kwa wananchi kwa uonezi wanaodai kufanyiwa ndani ya Bunge.
Wabunge walio katika ziara hiyo ni pamoja na mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa, mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi, mbunge wa ilemela Highness Kiwia, mbunge wa Nyamagana Ezekia Wenje, mbunge wa Ubungo John Mnyika, mbunge wa Singida mashariki Tindu Lissu, na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.
Akihutubia wananchi wa mkoa wa iringa katibu mkuu wa chama hicho dr slaa pamoja na kuzungumzia mambo mengi pia amezungumzia kesi inayomkabili Mkuu wa Kitengo cha Usalama, CHADEMA, Wilfred Rwakatare, ambapo amesema ni njama zinazopangwa kukichafua chama hicho kwa kuweka sauti kwenye picha za rwakatale alizopiga nyumbani kwake.
Amesema njama zote wameshazigundua na jinsi usalama wa taifa unavyotumika kwa kuwarubuni vijana wa chadema kuwanyofolea nyaraka mbalimbali katika ofisi zao, ikiwa ni pamoja na kuwahonga hela kiasi cha sh laki tano vijana wawili wa chama hicho ili kutoa ushaidi wa uongo katika kesi hiyo.
0 comments:
Post a Comment