Main Menu

Wednesday, April 17, 2013

BARUA ZILIZOTUMWA KWA BARAKA OBAMA ZAGUNDULIKA KUWA NA SUMU AINA YA RICIN

Barua zilizokuwa zimetumwa kwa Rais Obama na Seneta wa Mississippi, zilizobainika kuwa na  sumu hatari aina ya ricin zinahusiana. Idara kuu ya upelelezi ya Marekani FBI imetoa taarifa  hiyo.

Barua hizo zote zilitumwa kutokea Memphis, Tennessee.
Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 45 amekamatwa Mississippi kuhusiana na barua hizo.

Pamoja na barua hizo, polisi mjini Washington wanavichunguza vifurushi vitatu vya mashaka vilivyogunduliwa katika ofisi za majengo ya seneti.

Kugunduliwa kwa vifurushi hivyo kwenye eneo  kubwa la majengo ya serikali kumesababisha   wasiwasi,na idara za usalama zimeongeza ulinzi.

Barua kwa Rais Obama na Seneta Wicker zilitumwa tarehe 8 kabla ya mashambulio ya mabomu mjini Boston.

0 comments:

Post a Comment