Main Menu

Monday, April 29, 2013

AHUKUMIWA KWA KUFANYA BIASHARA HARAMU YA VIUNGO VYA BINADAMU

Mahakama ya Umoja wa Ulaya nchini Kosovo, leo imewahukumu adhabu ya hadi kifungo cha miaka minane jela, watu watano kwa tuhuma za kuuza viungo vya binadamu isivyo halali. 

Watu hao wanatuhumiwa kuuza viungo hivyo katika zahanati ya Pristina mwaka 2008. 

Miongoni mwa waliohukumiwa adhabu hiyo ni pamoja na daktari wa magonjwa ya kiume, Lufti Dervishi. 

Jaji kiongozi katika kesi hiyo kutoka Poland, Arkadiusz Sedek amesema kuwa watu hao watatumikia adhabu hiyo kati ya mwaka mmoja hadi miaka minane jela. 

Watuhumiwa wawili katika kesi hiyo iliyofunguliwa mwaka 2011, wamefutiwa mashtaka na kuachiwa huru.

0 comments:

Post a Comment