Main Menu

Friday, March 29, 2013

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI BBC WAGOMA KUPINGA KUPUNGUZWA KAZI



Wafanyakazi wa Shirika la Habari la BBC wamegoma kupinga mpango wa kufutwa kazi wafanyakazi katika shirika hilo.

Habari zinasema kuwa, waandishi wa habari na wafanyakazi kadhaa wa BBC jana walifanya mgomo wa masaa 12 kupinga mpango huo na kulalamikia mazingira magumu ya kazi zao.

Washiriki wa mgomo huo wametajwa kuwa, ni kutoka muungano wa Bectu na Muungano wa Taifa wa Waandishi wa Habari wa Magazeti ambao wamepinga vikali mpango wa kupunguzwa wafanyakazi katika shirika hilo.

Inatazamiwa kwamba, mgomo humo utaathiri kwa kiasi kikubwa matangazo ya moja kwa moja ya redio na televisheni ya Shirika hilo la Habari la BBC.

Zaidi ya wafanyakazi 2000 watalazimika kufutwa kazi katika kipindi cha miaka mitano ijayo, ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuwafuta kazi kwa lazima wafanyakazi wa shirika hilo.

0 comments:

Post a Comment