Main Menu

Wednesday, March 27, 2013

SIMBA, KAGERA SUGAR UWANJANI LEO




                                 WACHEZAJI NA VIONGOZI WASIMBA WAKIPIGA DUA
                                   KIKOSI CHA KAGERA SUKARI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaendelea leo kwa mechi mbili ambapo bingwa mtetezi Simba atakuwa mgeni ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.



Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 unatarajiwa kushuhudia mechi yenye ushindani kutokana na uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili.



Mechi nyingine itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam kati ya wenyeji Azam na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

0 comments:

Post a Comment