Main Menu

Wednesday, March 6, 2013

RAIS WA VENEZUELA HUGO CHAVEZ AFARIKI DUNIA



Rais wa Venezuela, Hugo Chavez, amefariki dunia baada ya kuugua kwa miaka miwili ugonjwa wa saratani na hivyo kufikisha ukingoni uongozi wake wa miaka kumi na nne katika taifa hilo la Amerika ya kusini lenye utajiri mkubwa wa mafuta. 

Makamu wa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, ametangaza kupitia kituo cha televisheni nchini humo kuwa Chavez mwenye umri wa miaka 58 ameaga dunia na kusema kifo chake kimewaacha na uchungu mwingi. 

Chavez amefariki katika hospitali ya kijeshi huko Caracass baada ya kuugua kwa muda  na kufanyiwa upasuaji mara nne uliosababisha afya yake kuzorota.

Serikali ya Venezuela imetangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa na kwamba Rais huyo atazikwa Ijumaa hii. 

Mwezi Oktoba mwaka jana Chavez alishinda uchaguzi lakini hali yake ya afya ilizorota kiasi cha kutoapishwa.

0 comments:

Post a Comment