Main Menu

Tuesday, February 26, 2013

RADIO IMAN, KWA NEEMA ZAFUNGIWA, CLOUDS FM YANUSURIKA.



Mamulaka ya mawasiliano nchini TCRA Imevifungia matangazo kwa muda wa miezi sita kuanzia leo vituo viwili vya radio na kingine kimoja kupewa onyo kali kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kurusha vipindi vinavyokiuka maadili ya utangazaji.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya maudhui TCRA Walter Bugoya amevitaja vituo vilivyofungiwa kurusha matangazo ni Radio Imani ya Morogoro, na kwa neema fm ya jijini mwanza huku kituo cha Clouds fm kikipewa onya kali na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 5.

Radio iman ya morogoro imefungiwa kwa kosa la kushawishi watu wasishiriki zoezi la sensa ya watu na makazi lililofanyika mwaka jana mwezi wa nane.

wakati radio kwa neema ya jijini mwanza yenyewe ikifungiwa kwa kushabikia malumbano ya uchinjaji yaliyotokea mkoani mwanza katika wilaya ya geita ambapo yalisababisha mauaji.


Amevitaka vituo vingine vya radio nchini kuwa makini katika vipindi vyao na kurusha matangaza kwa kuzingatia kanuni na maadili ya utangazaji

0 comments:

Post a Comment