Thursday, January 10, 2013
UCHAGUZI WA RAIS ZIMBABWE UENDA USIWE HURU
Rais wa zimbabwe robert mugabe
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetoa ripoti inayosema kuwa huenda uchaguzi mkuu wa rais nchini Zimbabwe usiwe huru kutokana na serikali ya nchi hiyo kushindwa kufanya marekebisho muhimu ya kisheria yanayoweza kuandaa mazingira mazuri ya kufanyika uchaguzi wa haki.
Ripoti hiyo imesisitiza udharura wa kufanyiwa marekebisho baadhi ya sheria za uchaguzi pamoja na taasisi muhimu ili kuepuka kujikariri machafuko ya kisiasa kama yale ya mwaka 2008.
Ripoti ya Human Rights Watch inasema makubaliano ya kugawana madaraka kati ya Rais Robert Mugabe na hayakuingizwa kwenye katiba na hivyo kufanya utekelezaji wake kutokuwa na ulazima wa kisheria.
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai
Miongoni mwa vipengee vilivyopuuzwa kwenye makubaliano hayo ni uundwaji wa katiba mpya ambayo mchakato wake umeendelea kusuasua hadi sasa. Uchaguzi mkuu wa Rais nchini Zimbabwe unatarajiwa kufanyika baadaye
chanzo radio tehrani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment