Main Menu

Saturday, January 26, 2013

SIMBA YAANZA KWELI ROUND YA PILI KWA KUIFUMUA A,LYON



      ngasa akipiga pushap baada ya kufunga bao la tatu

SIMBA SC leo imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa African Lyon ya Dar es Salaam mabao 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa duru ya pili.

Hadi mapumziko Simba SC tayari walikuwa mbele kwa mabao 3-0, yaliyotiwa kimiani na Mrisho Khalfan Ngassa mawili dakika za 19 na 39 na Ramadhan Suleiman Chombo ‘Redondo’ dakika ya tatu ya mchezo huo.

Redondo aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya tatu, akiunganisha krosi nzuri ya Ngassa kutoka wingi ya kushoto na kufumua shuti akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Lyon.

MATOKEO YA MECHI NYINGINE

Mtibwa Sugar 0-1 Polisi Morogoro

Coastal Union 3-1 Mgambo JKT

Ruvu Shooting 1-0 JKT RUVU

Azam FC 3-1 Kagera Sugar

JKT Oljoro 3-1 Toto Africans

KESHO; Januari 27, 2013

Yanga SC Vs TZ Prisons

0 comments:

Post a Comment