Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewasilisha barua ya malalamiko yake dhidi ya matumizi ya wachezaji wenye umrimkubwa na unyanyasaji uliofanyuwa kwa maofisa wa timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17 wa Serengeti Boys wakatiwa mechi ya marudiano ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana dhidi ya Congo.

Serengteti Boys iliondolewa kwenye mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi yakwanza iliyofanyika Novemba 18, 2012 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es salaam na baadaye kukubali kipigo cha mabao 2-0 kwenyemechi ya marudiano jijini Brazaville Jumapili iliyopita.

Hata hivyo, mechi hizo mbili zilizingirwa na matukio tata, hasa kuhusu umri wa wachezaji wa Congo ambao kimaumbile walionekanakuwa ni umri mkubwa zaidi na kusababisha TFF kuwasiliana na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuhusu njia zinazowezekanakupata uthibitisho wa umri wa wachezaji hao, lakini ilishindikana na ndipo TFF ilipocheza mechi hiyo ikiwa na imeweka pingamnizi.

Katika barua iliyotumwa CAF jana, TFF imerejea barua ya pingamizi aliyokabidhiwa kamisaa wa mechi ya kwanza jijini Dar Es salaam,Bw. Chayu Kabalamula na malalamiko yaliyowasilishwa kwa kamisaa wa mechi ya marudiano kuhusu vurugu walizofanyiwa maofisa watimu.

Katika barua hiyo, TFF imeomba CAF iagize kuwa wachezaji wote wa Congo waliocheza mechi hizo mbili wapimwe tena kwa kutumiakipimo cha M.R.I na gharama za zoezi hilo zilipiwe na TFF; na pili Shirikisho limeomba kuwa CAF ikubali kuipa Tanzania wiki tatu zakukusanya ushahidi na kuuwasilisha Cairo kwa ajili ya maamuzi.

Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, nchi shiriki zinatakiwa kuwapima wachezaji wake kwa kutumia kipimo cha M.R.I ambachokinaweza kutambua umri wa vijana walio chini ya miaka 17 na kwamba matokeo yake yanatumwa CAF, ambayo itahifadhi matokeo hayohadi hapo kutakapotokea pingamizi na ndipo itafanyia kazi kwsa kutoa matokeo ya vipimo hivyo.“Ni matumaini yetu kuwa suala letu litafanyiwa kazi na kutolwewa ufumbuzi ili kulinda soka la vijana barani Afrika dhidi ya vitendovilivyokomaa vya udanganyifu wa umri,” alisema katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana, kocha Jacob Michelsen alisema alishangaa kuona wachezaji wenye umrimkubwa zaidi wakichezeshwa kwenye mechi ya marudiano, lakini akaisifu TFF kuwa inafuata njia sahihi ya maendeleo na haina budikuendelea na programu yake ya soka la vijana.

"Najivunia vijana wangu kwa kuwa walijituma kwa muda wote pamoja na kwamba wenyeji waliongeza wachezaji wenye umri mkubwazaidi kuliko waliokuja huku," alisema kocha huyo kutoka Denmark.

"Kitu cha msingi ni kufuata njia sahihi ya kuendeleza soka na natumaini TFF iko kwenye njia sahihi na itaendelea na programu yake yavijana. Hakuna njia ya mkato kama mnataka maendeleo. Ni lazima tufuate njia sahihi na matunda yake tutayaona baadaye.

"Kila mara nasema mambo (ya vijana) huchukua muda mrefu (Things Take Time) na hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.

"Wenzetu walitumia njia za ajabu na hata hiyo penati ya bao la kwanza haikuwa faulo. Ilitokea nje kabisa ya eneo la penati. Refaalimuangalia kibendera akaona ametulia, akamuangalia beki mchezaji akamuona amesimama, mara akaangalia juu na kupuliza filimbikuonyesha kuwa ni penati."

Naye kocha msaidizi, Jamhuri Kihwelo alishindwa kujizuia na kujikuta akibubujika machozi wakati alipoelezea jinsi alivyoshambuliwa naaskari kabla ya mchezo huo.

 KOZI YA LESENI C KUFANYIKA ARUSHA

Kituo cha Kukuza Vipaji cha Rolling Stone kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimeandaa kozi ya leseni C yawalimu wa mpira wa miguu itakayofanyika kuanzia Desemba 10, 2012 hadi Desemba 23, 2012 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeidmjini Arusha.

Kozi hiyo itahusisha makocha walio na Cheti cha Kumaliza Elimu ya Sekondari au wale waliohitimu kozi ya ualimu wa mpira wa miguu yangazi ya kati (intermediate).

Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni alisema kuwa washiriki wa kozi hiyo wanatakiwa kuwa wamewasili Arusha ifikapoDesemba 9, 2012 na wanatakiwa kwenda na vyeti vyao halisi vya elimu. Alisema tayari Rolling Stone wameshasajili walimu 25 ambaowatashiriki kozi hiyo na hivyo kuwataka watu wengine wanye sifa kutoka mkoa wa Arusha na mikoa mingine kujitokeza kushirikimafunzo hayo muhimu.

Kayuni alisema kuwa kadri taifa litakavyozalisha walimu wengi, ndivyo taifa litakavyokuwa na uwezo wa kuandaa watoto na vijanawengi katika misingi sahihi ya mpira wa miguu na hivyo kuwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri.

Kozi hiyo itaendeshwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Kayuni kwa kushirikiana na mkufunzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu laAfrika (CAF), Bw. Dominic Niyonzima kutoka Rwanda.

Kwa mujibu wa Rolling Stone, kila mshiriki atajigharimia nauli ya kwenda Arusha na atatakiwa kwenda na ada ya fedha zinazolingana naDola 100 za Kimarekani (dola moja ni sawa na Sh1,580 za Tanzania).
Sita wapitishwa kuwania uongozi TAFCA

Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Waliku wa Mpira wa Miguu (TAFCA) imetangaza matokeo ya usaili wa wagombea uongozi chama hicho,ikiwa imepitisha wagombea sita sita na kuwaengua wagombea watano kwenye nafasi tofauti.

Baada ya usaili wa wagombea hao, Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA iliwaengua wagombea hao watano kwa kutokidhimasharti ya Ibara ya26 (2) ya Katiba ya TAFCA na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na pia kutokidhi utashi wa masharti ya 11 (1) yakanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

Katika nafasi ya mwenyekiti Oscar Don Korosso alipitishwa kuwa mgombea pekee baada ya Kenedy Mwaisabula na Jamhuri Kihwelokuenguliwa kwa kutokidhi masharti ya ibara ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na kanuni ya tisa ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

Katika nafasi ya makamu mwenhyekiti, Kamati imempitisha Lister J. Manyara kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo huku Marco Bundaraakipitishwa kuwa mgombea pekee wa nafasi ya katibu mkuu wa TAFCA.
Hali kadhalika wagombea wawili wa nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF, Wilfred Kidau na Magoma Rugora wamekidhi mashartiya Katiba ya TAFCA na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na hivyo watachuana kuwania kura za wajumbe wa mkutano mkuu,huku Ally A Mtumwa akienguliwa kwa kutokidhi masharti ya kanuni ya 11 (1) ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

Katika nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji, wagombea wote wawili, Abubakar Balingula na Aboubakar Salum wameenguliwa kwakutokidhi masharti ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba ya TAFCA na Kanuni ya 9 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)