Taarifa iliyotolewa
leo December 11. 2013 na Albert Msando ambae ni Mwanasheria wa Mbunge wa Kigoma
Kaskazini Zitto Kabwe kuhusu zile headlines za hivi karibuni za kuvuliwa vyeo
CHADEMA imesema ‘baada ya kupokea barua yake ya mashtaka 11 tarehe 01/12/2013
ambayo anashitakiwa nayo na iliyomtaka ajitetee kwa maandishi, Mheshimiwa Zitto
Zuberi Kabwe (MB) jana tarehe 10/12/2013 amefanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni za Uendeshaji za Chama’
Mheshimiwa Zitto
Zuberi Kabwe (MB) ametoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Chama kumueleza nia yake
kukata rufaa Baraza Kuu la Chama kupinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu
dhidi yake kumvua nyadhifa zake ndani ya Chama ambapo kuna sababu mbili za
msingi za kukata rufaa;
1. Utaratibu wa
kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa. 2. Sababu za kuchukuliwa hatua hizo sio
sahihi.
Utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu
kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji ni kama ifuatavyo;
Kanuni ya
Uendeshaji inasema kiongozi yeyote hatochukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza
kupewa mashitaka yake kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya
kujibu mashitaka kwa maandishi pia tunapenda ijulikane kwamba Kanuni ya
Uendeshaji 6.5.2 (a), (b), (c) na (d) kama ilivyorekebiswa Januari 2013
inasema;
Kwa mujibu wa ibara
ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu
ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza;
a) Kujulishwa
makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki
mbili.
b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada
ya kusikilizwa.
d)Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b),
(c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa
isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye
kikao husika.
Naomba nichkue
fursa hii kufafanua kuwa uongozi wa chama ulifanya mkutano na waandishi mnamo
tarehe 26/11/2013 na kusema kwamba marekebisho haya ya Kanuni ya mwaka 2013
ambayo nimewawekea hapo juu, ndiyo utaratibu waliofuata pia walieleza kuwa
sikuwa naifahamu na nilidanganywa kwani Kanuni ilishabadilishwa.
Mabadiliko haya
ambayo ni katika kipengele (d) kuhusu hatua ya dharura iliyochukuliwa na Kamati
Kuu haikugusa kipengele (a) cha Kanuni. Yaani ni kuwa hata kama Kamati kuu
itachukua hatua ya dharura kwa mujibu wa kipengele (d), bado kipengele (a) ni
lazima ifuatwe na inatamka wazi sharti la kiongozi kupewa mashtaka kwa
maandishi na kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi. Hii ni haki ya msingi kwa
kila utawala au uongozi.
Mheshimiwa Zitto
Zuberi Kabwe hakupewa mashtaka yake aliyakuta ndani ya kikao baada ya kupewa
taarifa kwa ujumbe wa simu (text message au sms) ambapo kwa uzito wa makosa
hayo yaliyosababisha kuvuliwa uongozi na kwa kuangalia athari zake kwake yeye
binafsi na chama kwa ujumla, Kamati Kuu ilitakiwa kujiridhisha kwamba Kanuni za
Uendeshaji na Katiba zinafuatwa.
Hili linaendana na
utaratibu uliotumika kwa Samson Mwigamba kuvuliwa nyadhifa yake ya uenyekiti wa
mkoa. Yeye hakuitwa kabisa kwenye kikao hicho na ni ukiukwaji wa Kanuni ya
Uendeshaji
6.5.6(d)
niliyoisoma hapo juu kwamba lazima kiongozi huyo aitwe kwenye kikao, sababu
zilizotumika ingawaje hajapokea taarifa rasmi ya maandishi kwa mujibu wa Kanuni
za Uendeshaji ni kwamba yeye ameshirki kwenye kuandaa na kusambaza waraka ambao
unasemekana ni mkakati wa ushindi wenye lengo la kupindua uongozi uliopo.
Waraka huo
haukumtaja Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kama muandaaji au msambazaji.
Waliouandaa hawajaukana na badala yake wamesema waziwazi kabisa kwa maneno na
maandishi kwamba Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe HAHUSIKI. Sio sawa kumuadhibu Mheshimiwa
Zitto Zuberi Kabwe kwa hisia au tu kwa sababu ya urafiki wake na watu fulani.
Haya ni mapungufu
ambayo kwa bahati nzuri Katiba na Kanuni za Uendeshaji zinatoa nafasi ya
kurekebishwa kwa kutoa nafasi ya kukata rufaa. Na utaratibu ni huu hapa Kwa ufupi,
Ibara 6.3.6(d) ya Katiba ya Chama kwamba “Kiongozi aliyechukuliwa hatua za
kinidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya
ile mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho”
Ibara 6.3.6(e) ya
Katiba ya Chama “Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini
tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu”
Kanuni za
Uendeshaji zinatoa UTARATIBU ambao unatakiwa ufuatwe ili kiongozi aliyeadhibiwa
aweze kutumia HAKI yake ya kukata rufani kwa maneno haya, kanuni ya 6.5.8 ya
Kanuni za Uendeshaji >> “Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi
wa maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumuwezesha kuamua kukata rufani au la”
Kanuni ya 6.5.9 ya
Kanuni za Uendeshaji >> “Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa
kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa
adhabu”
Kanuni ya 6.5.10 ya
Kanuni za Uendeshaji >> “Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika
kuandaa
taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo
lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha mamuzi”
Mpaka hivi sasa
hatujapokea taarifa kamili ya mwenendo wa shauri tokea kikao cha Kamati Kuu cha
tarehe 20-21/11/2013 Huo ndio utaratibu ambao Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe
ameamua kufuata kwa kuheshimu maamuzi ya Kamati Kuu lakini kukatia rufaa
maamuzi hayo. Kuheshimu maamuzi sio kuyakubali uhalali wake.
Kumekuwa na matukio
ya kusikitisha ambayo mengine yamefikia mahali kuwa fujo na vurugu ikiwa ni
pamoja na kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama ambapo baadhi ya vurugu hizo
zimehusishwa na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na baadhi ya watu.
Mheshimiwa Zitto
Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo yanayoendelea na anayakemea na
kuwashauri wanachama wote kuwa watulivu na kuendelea kuwaheshimu viongozi wa
kitaifa. Hatua zimeshachukuliwa kukata rufaa na ni imani yake kwamba Baraza Kuu
la Chama litatenda haki kwa kupitia rufaa yake na kutoa uamuzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment