Main Menu

Wednesday, April 17, 2013

MAELFU YA WAINGEREZA WAJITOKEZA ALIYEKUA WAZIRI WA KWANZA MWANAMKE NCHINI HUMO MARGARET THATCHER




Maelfu ya watu wamejipanga kandoni mwa barabara mjini London leo, kumuaga waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo Margaret Tatcher ambaye amezikwa leo. 


Watu hao walishangilia mwili wa marehemu ambao ulifunikwa na bendera ya Uingereza, na kubebwa katika gari lililovutwa na farasi sita weusi kutoka kanisa kuu la mtakatifu Paul hadi sehemu za mazishi.


 Wanajeshi 700 waliochaguliwa kutoka kikosi kilichopigana vita katika visiwa vya Falklands pia walijipanga kando kando mwa barabara. 


Askofu Richard Chartres aliyeongoza ibada ya mazishi amejizuia kutamka chochote kuhusu siasa za Tatcher, akisema kuna muda muhimu wa kufanya mjadala juu ya urithi wake kisiasa. 


Warithi wake wote katika wadhifa wa uwaziri mkuu, John Major, Tony Blair na David Cameron wamehudhuria mazishi. 

Malkia wa Uingereza Elizabeth wa 2,alikuwa miongoni mwa viongozi wengine ambao pia wamehudhuria mazishi ya Bibi Thatcher.

0 comments:

Post a Comment