Watu watatu wameuawa katika mlipuko wa bomu uliotokea huko kaskazini mwa Kenya.
Polisi ya Kenya imetangaza kuwa, mlipuko huo uliotokea kaskazini mwa nchi hiyo umesababisha vifo vya watu watatu wakiwemo askari polisi wawili na kujeruhi watu wengine kadhaa.
Duru za polisi hazikutoa maelezo zaidi kuhusiana na mlipuko huo.
Siku chache zilizopita ulitokea mlipuko katika kambi ya wakimbizi wa Kisomali ya Dadaab iliyoko mashariki mwa nchi hiyo ambao ulisababisha vifo vya watu wawili.
Kambi ya Daadab inawahifadhi wakimbizi wengi wa Kisomali na inahesabiwa kuwa moja kati ya kambi kubwa zaidi za wakimbizi duniani.
chanzo radio tehran

0 comments:
Post a Comment