kamanda wa polisi mkoani njombe fulgence ngonyani
Katika hali isiyo ya kawaida Mahabusu mmoja amekufa akidaiwa kujinyonga akiwa ndani ya mahabusu ya kituo cha polisi katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe,.
Kamanda wa polisi mkoani humo Fulgence Ngonyani amesema, tukio hilo limetokea januari 17 majira ya saa 11 jioni ambapo marehemu huyo, Chuki Smwa mwenye umri wa miaka 21, mkazi wa kijiji cha Isapilano alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za wizi.
Kamanda Ngonyani amesema, siku moja kabla ya tukio mtuhumiwa aliifikishwa kituoni hapo na wananchi wa kijiji cha Isapulano kwa tuhuma za kuvunja nyumba mbili tofauti ambapo aliiba fedha sh.ilingi elfu 18 na vocha za simu zenye thamani ya shilingi 4000, mali ya Mista Kasigula na Eutiko Mbilinyi.
Mtuhumiwa alikutwa na baadhi ya vitu vilivyodaiwa kuibwa katika nyumba hizo na kwamba wakati akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili ndipo alipoamua kujiua kwa kujinyonga akiwa ndani ya mahabusu.
kwa mujibu wa uchunguzi wa awali uliofanywa na daktari umebaini kuwa mtuhumiwa ambaye kwa sasa ni marehemu alijinyonga kwa kutumia mkanda wa kaptura aliyokuwa ameivaa wakati akiingia mahabusu.

0 comments:
Post a Comment