KATIKA
hali isiyo ya kawaida, katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Jackob
Nkomola amefanya vurugu katika Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa , kwa kumvamia Mwandishi wa habari kwa kile alichokiita ni hasira ya
kesi yake.
Tukio
hilo limetokea Leo majira ya saa tatu na nusu katika Mahakama ya Mwanzo
iliyopo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, baada ya katibu huyo kusomewa
shtaka na hakimu wa Mahakama hiyo ya mwanzo Mh. Zakaria Mushi.
Akisoma
shtaka hlililomfikisha mahakamani hapo hakimu Mushi alisema mtuhumiwa Jackob
Nkomola anashtakiwa kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno, na hivyo kuvunja
sheria kifungu namba 89 kifungu kidogo “A”.
Aidha
hakimu huyo alisema mshitakiwa alitenda kosa hilo, siku ya tarehe 3 mwezi wa
kumi mwaka 2012 katika eneo la Mkombwe, ambapo alimtishia Alexandel Tweve
mkazi wa Mafinga.
Mtuhumiwa
alikana shtaka hilo na hakimu kutoa masharti ya dhamana ya ahadi ambayo inathamani
ya shilingi Laki mbili, na adhaminiwe na mtu mmoja atakayetambulishwa kwa
barua kutoka katika ofisi ya serikali ya kijiji au Kata.
Kupitia
masharti hayo mshatakiwa alikuwa na mdhamini ambaye hakukidhi vigezo vya kuwa
na barua ya uthibitisho kutoka katika ofisi za serikali ya kijiji na
hivyo kuzuiliwa kwa muda wa saa moja akiwa chini ya ulinzi, hadi kesi
itakaposikilizwa tarehe 30 mwezi huu wa kwanza 2013.
Hakimu
alimtaka mstaki wa kesi hiyo kufika na mashahidi wake aliowaorodhesha, na
baada ya mwandishi wa gazeti hilo kutoka nje kwa ajili ya kupiga picha,
mtuhumiwa alimfuata mwandishi na kumkuda akihoji ridhaa ya mwandishi huyo
kupiga picha.
“Kwa
nini unanipiga picha?? Nani amekuruhusu unipige picha, kwanza wewe ni nani??,
umepokea rushwa huko uje uniandike mimi, na nitaona kama habari hiyo itatoka,”
Alihoji Katibu huyo.
Akijibu
maswali ya mtuhumiwa huyo mwandishi alisema “Mimi ni mwandishi wa habari,
nimepata ruhusa kutoka kwa hakimu wa mahakama hii kufanya kazi yangu, na
sijakupiga picha wewe, bali nilikuwa ninapiga picha ya kibao cha mahakama na
jingo,”.
Hatua
hiyo iliwashangaza watu waliohudhuria kesi hiyo katika viunga vya mahakama
hiyo, wakihoji mamlaka ya mtuhumiwa kumfuata umbali wa hatua zaidi ya tano
mwandishi, huku mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi kwa kuwa bado alikuwa
naashikiriwa na Mahakama hiyo kwa kutokidhi vigezo vya dhamana yake.
Mwandishi
alikimbilia kwa hakimu wa mahakama hiyo akitaka msaada juu ya tujkio hilo, na
ndipo hakimu Mushi alimtaka mwandishi huyo kufika kituo cha polisi kutoa
taarifa ya tukio hilo.
Akiwa
njiani Mwandishi alimpigia simu Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi Cosmas
Kaguo ambaye alimuomba mwandishi kuonana naye kabla ya kufika katika kituo cha
Polisi cha Mafinga.
Hatua
ya mwenyekiti wa CCM Kaguao, - aliitisha kikao cha dharua cha kamati ya siasa
na kuomba radhi juu ya tukio lililotokea, na baada ya muda dakika 20 Katibu wa
CCM (Mtuhumiwa) aliingia katika moja ya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi, iliyopo katika ukumbi wa mikutano na kuomba radhi juu ya kile
alichokifanya katika viunga vya mahakama.
Ombi
la mwenyekiti wa CCM Wilaya, lilikubaliwa na mwandishi huyo kwa kusitisha hatua
yake ya kufungua kesi katika kituo cha polisi Mafinga.
Akitoa
utetezi wake, mtuhuimiwa huyo alisema “Ninaomba unisamehe sana Oliver, unajua
kesi yangu hii niya kisiasa, na kukufanyia hivyo ni hasira baada ya mtu
anayenituhumu kutumia njia mbalimbali za kuniangamiza, ninajua nimekukwaza
wewe, lakini pia nimeidhalilisha taaluma yako, ninakuomba unisamehe,” Alisema
Nkomola.
Hata
hivyo wachagizaji wa masuala ya siasa Wilayani humo walisema katibu huyo
amekuwa akitumia vibaya wadhfa alionao, na kujisahau kama kuna mikono ya sheria
, na kuwa nguvu ya kufanya vurugu katika chombo hicho cha mahakama ambacho ni
muhimili mkuu wa serikali, ni kutokana na jingo la Mahakama hiyo kuwa ni mali
ya chama cha mapinduzi.
Kikao
hicho cha usuruhishi dhidi ya tukio hilo, kilichukua zaidia ya saa nzima hadi
kumalizika kwake, mwandishi huyo yupo wilayani humo kwa siku ya tatu sasa,
akifuatilia masuala ya elimu kwa wanafunzi wanaoanza elimu ya kidato cha
kwanza, pamoja na changamoto zinazoikabiri sekta ya elimu na Kilimo Wilayani
humo.
0 comments:
Post a Comment