Main Menu

Monday, June 1, 2015

MABANK NCHINI ENGLAND KUCHUNGUZWA SAKATA LA RUSHWA LINALOWAHUSU MAAFISA WA FIFA



 Corinne Blatter sits with her father during the 65th FIFA Congress at the HallenstadionBenki mbili nchini Uingereza zimeanzisha uchunguzi wa akaunti zinazohusishwa na Shirikisho la soka duniani FIFA.

Benki za Barclays, Standard Chartered, na HSBC, zimetajwa katika ripoti ya idara ya ujasusi ya Marekani FBI kuwa zilitumika kufanikisha malipo ya kiinua mgongo na rushwa kwa maafisa wakuu katika FIFA.

Ripoti hiyo ndiyo iliyotumika kuwakamata maafisa wakuu 7 wa FIFA juma lililopita walipokuwa wamewasili mjini Zurich Uswisi kwa kongamano la kila mwaka la FIFA.

Kongamano hilo, lilimchagua rais wa FIFA Sepp Blatter kuhudumu kwa muhula wa 5 licha ya shinikizo kutoka kwa wadau wakimtaka ajiondoe ilikuruhusu uchunguzi wa kina kuhusu madai ya ufisadi unaoendelea ndani ya FIFA.

Benki za Barclays na HSBC zimekataa kujadili swala hilo huku benki ya Standard Chartered ikikiri kuwa inaendesha uchunguzi wa kina ili kubaini iwapo malipo hayo ya mlungula yalipitia ndani ya akaunti zake.

0 comments:

Post a Comment