Main Menu

Friday, May 15, 2015

PETR CECH AFUNGULIWA MILANGO YAKUONDOKA

 
Klabu ya Chelsea imesema kuwa kipa wake namba mbili msimu huu Petr Cech yupo huru kuongea na klabu yoyote inayotaka kumsajili.

Cech alijiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2004 akitokea klabu ya Rennes ya nchini Ufaransa na kufanikiwa kuchukua mataji mengi akiwa na Chelsea.

Ujio wa kipa aliyekuwa kwa mkopo katika klabu ya Atletico Madrid Thibaut Courtois kunako klabu ya Chelsea, umemlazimu kocha wa Chelsea Jose Mourinho kumtumia Cech kama kipa namba mbili.

Wakala wa Petr Cech Viktor Kolar amesema mteja wake anawaniwa na vilabu vingi vikiwepo vilabu vya Arsenal, Inter Milan, Besiktas na Liverpool.

Katika maisha yake kunako klabu ya Chelsea, Petr Cech amefanikiwa kuchukua makombe ya Ligi Kuu ya soka nchini England, Kombe la FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League.

0 comments:

Post a Comment