Main Menu

Friday, May 15, 2015

DANNY WELBECK KUIKOSA MAN U JUMAPILI



Welbeck scored for Arsenal in their FA Cup victory at Manchester United earlier this season Kuelekea michezo ya mwishoni mwa juma ya Ligi kuu ya soka nchini England, klabu ya Arsenal imesema kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Danny Welbeck hatokuwepo katika mchezo wa Ligi siku ya Jumapili dhidi ya Manchester United.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema hayo katika mkutano na waandishi wa Habari ikiwa ni siku mbili kuelekea katika mchezo huo.

Amesema Matatizo ya goti yanaweza kuwa sababu ya Welbeck kutokujumuishwa katika kikosi cha Arsenal kitakachowavaa Manchester United siku ya Jumapili.

Mara ya miwsho kwa Welbeck kucheza ilikuwa ni mwezi uliopita dhidi ya Chelsea katika sare ya bila kufungana.

0 comments:

Post a Comment