Timu ya
soka ya yanga ambao ndio wawakilishi pekee wa nchi katika michuano ya kimataifa
katika kombe la shirikisho kesho wanatarajia kuwafuata wapinzani wao nchini Zimbabwe.
Kwa mujibu
wa katibu mkuu wa timu hiyo Dr. Jonas Tiboroha timu hiyo inatarajia kuondoka
majira ya saa nne asubuhi kuelekea Bulawayo kabla ya kuifuata timu ya platinum katika
uwanja
Mandava uliopo mji wa Gweru.
Baada ya
yanga kupata ushindi katika mchezo wa kwanza kwa mabao 5-1 majuma matatu
yaliyopita ilitangaza kuondoka mapema kuifuata timu hiyo ili kuepuka usumbufu
walioupata timu ya sofa paka pindi walipowafuata platinum.
Lakini baadae
timu hiyo ilibadili ratiba ya safari yake na kuamua kuondoka siku moja kabla ya
mchezo huo hali ambayo inatoa wasiwasi kwa wapenzi wa timu hiyo kama kweli
inaweza kufanya vizuri na kusonga mbele.
Kwa mazingira
ya safari hiyo inaonesha yanga haitapata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye
uwanja watakaoutumia siku ya jumamosi hali ambayo inaweza ikawaathiri.
Timu ya
platinum ni timu ya mgodi kama ilivyo kwa timu ya mwadui ya mkoani shinyanga na
mchezo huo utapigwa mgodini ambapo ukaguzi huwa wa hali ya juu jambo ambalo
linaweza kuwaathiri wachezaji ikizingatiwa watafika siku hiyo hiyo ya mchezo.
Hazina ya ushindi
wa mabao 5-1 iliyonayo yanga inaweza kuwa ndio iliyowapa kiburi hicho cha
kuchelewa kuwafuata wapinzani wao japo kama wao waliweza kushinda 5 nyumbani Platinum
wanashindwaje kushinda 4 nyumbani?
Mashabiki wa
timu hiyo wao walitangulia na basi tangu siku ya jumanne wakiongozwa na mkuu wa
kitengo cha habari na mawasiliano Jerry Murro.
Endapo
yanga itafanikiwa kuitoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na
itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du
Saleh ya Tunisia.
0 comments:
Post a Comment