Main Menu

Wednesday, March 4, 2015

YANGA BADO YALIA NA BODI YA LIGI NA TFF, YAAPA KUTOPELEKA TIMU TAREHE 11



PRESS RELEASE
Uongozi wa klabu wa ya Yanga umebaini upotoshaji na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kanuni na taratibu za uendeshaji za ligi unaofanywa na baadhi ya viongozi bodi ya ligi Nchini.

Katika uchunguzi tulioufanya tumebaini yafuatayo:-
1.    Ukweli kuhusu kadi za njano alizopata mchezaji wa simba IBRAHIM HAJIB MIGOMBA,mchezaji huyu tumebaini kuwa alipata kadi nne za njano katika michezo minne aliyecheza tazama kiambatanisho nyuma ya taarifa hii.

2.    Barua iliyotolewa na bodi ya ligi nakusainiwa na Kaimu Afisa mtendaji mkuu FATMA ABDALAH kuidhinisha kuanza kutumiwa kwa kanuni mpya ya kumruhusu mchezaji husika kuchagua mechi ya kucheza au kutocheza  haikuwa sahihi kutokana na marekebisho hayo kutoanza kutumika.

Tulichobaini ni kuwa ili mapendekezo ya kanuni hizo yaanze kutumika sheria inataka raisi wa Tff na katibu mkuu wa Tff kuzisaini ili ziwe rasmi kutumika jambo ambalo uchunguzi wetu umebaini kuwa  raisi wa Tff bado hajazisaini ili ziweze kutumika japo zimepitishwa na kamati ya utendeji wa Tff,ili kanunu na taratibu izo zianze kutumika  sheria inamtaka raisi  na katibu wa Tff kuzisaini ili kualalisha  matumizi yake na si vinginevyo .

3.    Upotoshwaji wa taarifa za kuarishwa kwa mchezo wetu na Jkt ruvu ,akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari Kaimu Afisa mtendaji mkuu  wa bodi ya ligi Fatmah  Abdala alikaririwa akisema uongozi wa yanga uliarifiwa kwa barua pepe  tangu tarehe 16/02/2015  ukweli katika hili hatukupata taarifa yeyote ya kuarishwa kwa mchezo wetu na kwa mujibu wa taratibu na kanuni za ubadilishaji wa Ratiba bodi yaligi inapaswa kukaa na timu husika na kujadili marekebisho ya mchezo husika jambo ambalo bodi ya ligi haikulifanya wakati wanaarisha mchezo wetu na Jkt ruvu ambao ulikuwa uchezwe leo .

TUNACHOPENDEKEZA
1.    Shirikisho la mpira wa miguu TFF  kuingilia kati utata huu kwa kuipokonya klabu ya simba pointi 3 ilizozipata kwenye mchezo wake na prisons  mechi namba 125
2.    Kutoa adhabu kali kwa viongozi wa simba na mchezaji husika kwa kukiuka kanuni na taratibu za uendeshaji wa ligi .
3.    Tunamtaka Kaimu Afisa mtendaji wa bodii Fatmah Abdala ajiuzulu kutokana na kupindisha sheria na taratibu na pia kupotosha umma wa watanzania kuhusu  sheria na pia kwa kutoa kibali hewa chakuruhusiwa kwa mchezaji HAJIB IBRAHIM Kucheza na prisons uko akiwa na kadi nne za njano

 Imetolewa  Na Idara Ya Habari Na Mawasiliano Ya Yanga
Jerry Murro 

 CHATI YA MECHI ALIZOPEWA KADI IBRAHIM AJIB

MATCH NO

DATE


GAME

STADIUM

17

4/10/2014

SIMBA VS STAND UNITED

TAIFA      –DAR ES SALAAM

99

15/2/2015

POLISI MOROGORO VS SIMBA

JAMUHURI- MOROGORO

108

22/02/2015

STAND UNITED VC  SIMBA

KAMBARAGE -SHINYANGA

125

28/2/2015

SIMBA VS TZ PRISONS

TAIFA  –DAR ES SALAAM

0 comments:

Post a Comment