Main Menu

Tuesday, March 3, 2015

MAANDALIZI YA SPORTS XTRA DAY BONANZA 2015 YAANZA, MABINGWA WATETEZI WATHIBITISHA USHIRIKI MIKOA YOTE.


Homa ya Bonanza la Sports Extra Day….. au Sports Kazini Mwezi Mei… imeanza kupamba moto, makampuni mengi yameanza maandalizi mapema kujiandaa na bonanza hilo maarufu hapa nchini linalodhaminiwa na Clouds Media Group. 

Timu ya Tanesco ambao walikuwa mabingwa wa bonanza hilo mwaka 2013 watacheza mechi ya kirafiki na timu ya Clouds Dream team siku ya jumamosi wiki hii, Clouds pia wanajiandaa na mashindano makubwa ya NSSF Media Cup 2015 yanayotarajiwa kuanza wiki ijayo tarehe 14. 
 
Mchezaji wa timu ya fastjet mabingwa wa mwaka jana akichuana na mchezaji wa tanesco mabingwa wa mwaka juzi.
 
Timu za Fastjet ambao ni mabingwa watetezi wao wamethibitisha kushiriki katika mikoa yote mwaka huu. 

Bonanza hilo ambalo ni maalum kwa ajili ya wafanyakazi litafanyika tarehe moja mei hapa Dar Es Salaam, ikifuatiwa na Mwanza, Arusha na Mbeya kila mwisho wa wiki katika mwezi mei 2015.


 Peter Ngassa
Managing Director

Butterfly logo

+255 752 716 636

0 comments:

Post a Comment