Main Menu

Wednesday, February 25, 2015

USIKU WA ULAYA, WENGER KUIKABILI TIMU YAKE YA ZAMANI...BAYER 04 VS ATLETICO

Baada ya kushuhudia michezo ya hapo jana katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, michezo mingine ya hatua ya 16 bora itapigwa tena hii leo ambapo Arsenal watakuwa nyumbani kucheza na Monaco katika pambano litakalopigwa katika uwanja wa Emirates.

Mchezo huo utakuwa wa hisia kubwa sana kwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwani amekwisha wahi kuifundisha timu ya Monaco kuanzia mwaka 1987 na 1994 huku akishinda vikombe vya Ligi kuu ya soka nchini Ufarana na kombe la Ligi la Ufaransa maarufu kama Coupe De France.

Arsenal wataingia uwanjani pasipokua na nyota wake Aaron Ramsey ambaye ni majeruhi, Abou Diaby, Jack Wilshere na Alex Chamberlain wakati  Monaco wao watawakosa Toulalan na Traore.
Mchezo mwingine utakuwa kati ya Bayer 04 Levekusen dhidi ya Atletico Madrid.
Arsene Wenger is preparing to face his former club Monaco, where he is still remembered fondly
Arsene Wenger akijiandaa wakati akiwa meneja wa club Monaco, hii leo wanakutana.
The Frenchman looked relaxed ahead of Arsenal's most straightforward last-16 tie in several years
Wenger akiwa na furaha ya kukutana na timu yake ya zamani katika hatua ya 16 ya Uefa champions ligi.
Wenger is still Monaco's longest-serving manager after spending seven years in the principality
Wenger wakati anaihudumia Monaco enzi hizo

0 comments:

Post a Comment