Main Menu

Wednesday, August 20, 2014

SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI LATOA RATIBA YA LIGI KUU, AZAM KUANZA NA POLISI MORO

Shirikisho la soka nchini TFF leo limetoa ratiba ya michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza tarehe 20 ya mwezi wa tisa.
 
Ratiba hiyo imezingatia michuano ya Chalenji itakayochezwa mwezi Novemba, usajili wa dirisha dogo ambao utaanza Novemba 15 hadi Desemba 15, ushiriki wa klabu za Azam na Yanga kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa afrika na Kombe la Shirikisho.
 
Mechi za ligi msimu ujao zitachezwa wikiendi tu ili kuongeza msisimko na kuwapa fursa washabiki wengi zaidi kuhudhuria, katikati ya wiki imeachwa wazi kwa ajili ya mechi za Kombe la FA (Federation Cup), Vilevile kutakuwa na mechi Boxing Day na siku ya Mwaka Mpya.
 
Ratiba hiyo inaonesha mabingwa watetezi azam fc wataanza na wageni wa ligi Polisi Morogoro wakati Yanga wao wataanza ugenini dhidi ya Mtibwa Suger.
 
Simba sc wao wataanza dhidi ya Coastal Union jijini Dare s salaam wakati Ndanda Fc wao watafungua dhici ya Stand United mkoani Shinyanga.

0 comments:

Post a Comment