Main Menu

Friday, September 6, 2013

VIONGOZI WA G20 WATOFAUTIANA KUHUSU HALI YA SYRIA

Mkutano wa nchi 20 zenye uwezo mkubwa kiuchumi duniani, G20, unaingia siku yake ya pili na ya mwisho leo huko St Petersburg nchini Urusi huku viongozi wa ulimwengu wakisalia kutofautiana kuhusu mzozo wa Syria. 


Rais wa Marekani, Barrack Obama, anatafuta uungwaji mkono kutoka kwa viongozi wengine kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Syria lakini China na Urusi zimeionya Marekani kutochukua hatua yoyote bila idhini ya umoja wa Mataifa. 

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, alitenga muda jana kwenye dhifa ya chakula cha jioni kuzungumzia mzozo wa Syria licha ya kuwa haikuwa kwenye ajenda ya mkutano huo wa G20. 

 
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema hali ya Syria inasalia kuwa doa katika dhamiri ya ulimwengu na kwamba mzozo wa Syria ndio janga kubwa la kibinaadamu kwa wakati huu.


Utawala wa Syria unashutumiwa kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia tarehe 21 mwezi uliopita ambapo kiasi ya watu 1,400 waliuawa. 


Pembezoni mwa mkutano huo wa G20, msemaji wa rais Putin alipuuzilia mbali ripoti ya kijasusi ya Marekani kuhusu shambulio hilo lililofanyika Damascus.

NA dwswahili

0 comments:

Post a Comment