Maafisa wa kijeshi wa Umoja wa Mataifa na wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema kuwa kikosi hicho cha uingiliaji kati ambacho kina mamlaka makubwa ikilinganishwa na vikosi vingine vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, kinalisaidia jeshi la Kongo katika mapambano yake dhidi ya waasi wa M23.

Kanali Olivier Hamuli msemaji wa jeshi la Kongo amesema kuwa kikosi cha mapambano cha Umoja wa Mataifa kiko upande wao na kwamba kinawapatia silaha vikosi vya Kongo.
Raia wa Kongo wasiopungua wanne waliuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya nyumba kadhaa katika maeneo ya raia huko Goma kuangukiwa na makombora juzi Alkhamisi.
na radio tehran
0 comments:
Post a Comment