Main Menu

Tuesday, August 13, 2013

RAIS WA CLUB YA SEVILLA AGOMA KUMUUZA KONDOGBIA.



Rais wa klabu ya Sevilla Jose Maria del Nido ameviambia vilabu vinavyomuwania kiungo Geoffrey Kondogbia  kuwa nyota huyo hayupo kwenye mipango ya kuuzwa.

Kondogbia mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akitajwa kutakiwa na vilabu vingi thamani yake imetajwa kufikia Euro milioni 20 kama atahama Sevilla.

Kondogbia ambaye ni mmoja ya wachezaji waliotwaa taji la vijana na timu ya taifa ya Ufaransa mwishoni mwa wiki iliyopita aling’ara  kwenye mechi ya kumpongeza nyota  Rio Ferdnand ambapo Sevilla iliifunga Manchester united magoli 3-1.

Vilabu vya Manchester united , Chelsea, Real Madrid na Juventus vinamtaka kiungo huyo anayefananishwa uchezaji wake na kiungo wa Manchester City Yaya Toure.

 NA MVP Issa maeda wa ebony fm

0 comments:

Post a Comment