Main Menu

Friday, August 23, 2013

PUTIN APIGA MARUFUKU MAANDAMANO WAKATI WA MICHEZO YA OLIMPIKI MWAKANI

 
Rais Vladimir Putin wa Urusi amepiga marufuku maandamano wakati michezo ya Olimpiki ya msimu wa majira ya baridi kwa mwaka ujao wa 2014.  


Katika kufanikisha utekelezaji wa amri hiyo watu mbalimbali kuanzia katika viwanja vya michezo, bandari, vituo vya treni na vituo vya ukaguzi wa barabarani ambavyo vitakuwa maeneo muhimu ya ukaguzi watakaguliwa na  pamoja na mizigo yao. 
 
Amri hiyo ya rais ambayo imechapishwa katika gazeti la serikali Rossiyskaya Gazeta imeweka maeneo maalumu ya usalama katika jimbo la Sochi wakati wa  michezo hiyo mwezi wa Februari katika eneo la mapunziko la bahari Nyeusi. 


Amri hiyo pia imeweka "ukanda wa marufuku" kwa kuzuia kuingia  katika maeneo  ya  michezo  ya Olimpiki pamoja  na  sehemu  kubwa ya  mji  wa Sochi.


Aidha amri hiyo imepiga marufuku kuvuka mpaka na kuingia katika eneo la waasi la Abkhazia nchini  Georgia, ambalo lipo umbali wa kilometa kadhaa kutoka katika uwanja wa michezo ya Olimpiki.


 Mpango wa Putin umezuia maandamano yoyote ambayo hayahusiani na michezo ya Olimpiki katika eneo husika kuanzia Januari 7 mpaka Machi 21, 2014.

0 comments:

Post a Comment