Mfanyakazi wa zamani katika shirika la upelelezi la Marekani Edward
Snowden ameomba hifadhi ya muda nchini Urusi, ambako amekuwa
akiishi kwa wiki tatu zilizopita.
Idara ya uhamiaji ya Urusi ilithibitisha
jana kuwa imepokea maombi ya raia huyo wa Marekani, ambaye
amekwama katika uwanja wa ndege wa Moscow.
Hayo yameripotiwa siku chache baada ya Snowden kukutana na
wanaharakati wa haki za binadamu, na kutangaza nia yake ya
kuomba hifadhi ya muda nchini Urusi, kabla ya kuhamia katika nchi
za Amerika Kusini zilizompatia hifadhi ya ukimbizi.
Marekani imekwishaifuta pasipoti ya Snowden, na inafanya kila
juhudi kumkamata na kumfungulia mashitaka ya ujasusi, baada ya
kufichua mpango wa nchi hiyo kuchunguza mawasiliano ya watu
binafsi na nchi washirika.
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema
Urusi itampa hifadhi Snowden, ikiwa ataacha mienendo inayoweza
kuharibu uhusiano wa Urusi na Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment