Main Menu

Tuesday, July 23, 2013

Dkt. KAWAMBWA ATEMBELEA OFISI MPYA ZA BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa na Naibu wake Mhe. Philipo Mulugo wametembelea Ofisi Mpya za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zilizopo Mwenge Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam.

 Katika ziara hiyo Mhe. Dkt. Kawambwa aliongozana na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo akiwemo Kaimu Katibu Mkuu Bw. Selestine Gesimba, Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Prof. Sylvia Temu na Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Tarimo. 

Akiwakaribisha katika Ofisi hizo Bw. George Nyatega, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, alisema sababu kuu ya kuhama Ofisi za awali ni kutokana na taasisi kuzidi kuwa kubwa na kwamba idadi ya wafanyakazi imeongezeka na hivyo ilitakiwa kupata ofisi kubwa ili kuboresha huduma kwa wadau wake.

 Mhe. Dkt. Kawambwa ameipongeza Menejimenti ya Bodi ya Mikopo kwa hatua hiyo na pia kwa namna ambavyo imeboresha huduma katika miaka ya hivi karibuni. Aidha ameiagiza Menejimenti ya Bodi hiyo kutobweteka na mafanikio yaliyopatikana badala yake iendelee kutoa huduma kwa ufanisi na weledi mkubwa katika mwaka wa masomo unaokuja wa 2013/2014 ili kuepusha migogoro ya wanafunzi kuhusu mikopo. 

 Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Ofisi ya Makao Makuu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imehama kutoka Msasani Tirdo Complex, Dar es Salaam ilipokuwa awali tangu kuanzishwa kwake Julai 2005.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) na Naibu wake Mhe. Philipo Mulugo wakifuatilia Kwa umakini Taarifa ya Menejimenti ya Bodi ya Mikopo Iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Bw. George Nyatega (hayupo pichani).
Mhe. Dkt. Kawambwa wa pili Kushoto akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Bw. Nyatega (aliyevaa koti la khaki) namna uchambuzi wa fomu za waombaji mikopo inavyofanyika, Pembeni aliyeshika Moja ya fomu za waombaji ni Naibu Waziri Mhe. Philipo Mulugo..
Menejimenti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Ikimkaribisha Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo Ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo (katikati) katika Ofisi Mpya za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu zilizopo Mwenge Barabara ya Sam Nujoma, Dar es Salaam. 

na michuzi blog


0 comments:

Post a Comment