Kundi la uangalizi wa uchaguzi la Umoja wa Ulaya limesema
leo kuwa uchaguzi mkuu wa Kenya wa Machi 4 ulikuwa wa
mafanikio lakini kuna somo linalopaswa kuzingatiwa kutokana na
matatizo yaliyojitokeza katika mchakato mzima wa uchaguzi.
Ripoti hiyo iliyotolewa leo mjini Nairobi imesema kuwa zoezi la
kutoa matokeo limeshundwa kuonyesha uwazi, wakati mawakala
wa vyama na waangalizi wa uchaguzi hawakupewa uwezo wa
kutosha kuona utaratibu wa kuhesabu kura katika vituo vya
kuhesabia kura.
Ikizungumzia kuhusu matokeo ya rais ripoti hiyo
inasema waangalizi walisifu kazi iliyofanywa na mahakama na
kuongeza kuwa uhuru wa taasisi hiyo ulikuwa muhimu kwa ajili
ya kufanikisha uchaguzi huo.
Kundi hilo la uangalizi wa uchaguzi limejadili mapendekezo yake
na waziri wa mambo ya kigeni Amina Mohammed , mgombea wa
urais kwa tikiti ya chama cha CORD Raila Odinga, mwenyekiti
wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka Issack Hassan
pamoja na wadau wengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment