Main Menu

Thursday, May 30, 2013

MWANDISHI WA HABARI NCHINI SOMALIA ASHAMBULIWA KWA RISASI NA KUJERUHIWA

Nchini Somalia, watu waliokuwa na silaha wamempiga risasi na kumjeruhi mwandishi habari mmoja katika mji wa bandarini wa Kismayo  katika msururu wa mashambulio dhidi ya wanahabari nchini humo.

Kulingana na wanahabari wenzake na maafisa wa usalama, washambuliaji wasiojulikana walimpiga risasi Abdirasak Sofe ambaye anajulikana kwa jina la utani kama Jijile anayefanya kazi na kituo cha televisheni cha Royal kilicho na makao yake mjini London Uingereza alipokuwa akitembea kutoka kazini kuelelekea nyumbani jana jioni.

Ali Mohammed aliyeshuhudia shambulio hilo alisema watu wawili mmoja akiwa na bunduki aina ya AK 47 walimfyatulia risasi mwandishi huyo. 

Mwaka huu  pekee, hadi sasa jumla ya waandishi habari wanne wameshauawa nchini Somalia.

0 comments:

Post a Comment