Main Menu

Thursday, April 18, 2013

WANANCHI WA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, WAMETAKIWA KUTUMIA FURSA YA UTALII KUJIONGEZEA KIPATO

Afisa utalii Tanapa kanda ya Kusini Iringa Risala Kabongo

Wananchi wa mikoa ya nyanda za juu kusini hususani mkoa wa iringa, wametakiwa kutumia fursa ya vivutio vilivyopo ukanda huo kujiongezea kipato na kuweza kukabiliana na changamoto za maisha magumu zinazowakabili.

Wito huo umetolewa na afisa utalii TANAPA ofisi ya kanda ya kusini Iringa Risala Kabongo wakati akizungumza na mtandao huu ofini kwake kuhusiana na hali ya utalii ukanda wa kusini.

Wito huo umekuja kufuatia kasumba ilioyojengeka kwa watanzania wengi kuwa utalii ni kwa watu wa kigeni pekee na  kutembelea mbuga za wanyama basi, wakati hiyo sio maana halisi ya utalii.

Risala amesema mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa ya Tanzania iliyojaliwa vivutio vingi ambavyo vikitumiwa vizuri vitasaidia kuliongezea taifa kipato pamoja na wananchi wake.

Risala ametolea mfano zao la uyoga linalolimwa mkoani Iringa kuwa likitumika vizuri linaweza kuwaongezea kipato wananchi, pia ameyataja mazao kama ya matikiti ambayo yanapatikana kwa wingi mkoani humo mbali na kuwa kivutio kwa wageni waendao hifadhi ya ruaha lakini ni biashara ambayo ikiboreshwa itawakomboa wananchi.

Aidha risala amevitaja vivutio vingine ambavyo wananchi wanaweza kutembelea mbali na hifadhi ya ruaha kuwa ni jiwe la gangilonga lililopo manispaa ya iringa.

''kwa mfano jiwe la gangilonga pale unaweza ukaenda na familia yako siku za wikiendi na kuenjoy kwa kuiona madhari nzuri ya manispaa ya iringa kutokea pale na hata kupiga picha'' alisema Risala.

Ameongeza kuwa '' kaburi la mkwawa ilililopo kijiji cha kalenga ni moja ya vivutio ambavyo mtu anaweza kwenda na si kuangalia tu, pia kujifunza historia ya kiongozi huyo wa kihehe mwenye historia kubwa'' alisema.

Hata hivyo afisa huyo amewataka watanzania kutumia fursa iliyopo hivi sasa ya gharama za kutembelea hifadhi ambzo ni shilingi elfu moja kwa mtu mkubwa na shilingi mia tano kwa watoto, kabla ya gharama hivo hazijapandishwa mwezi wa saba.

''Gharama za kutembelea hifadhi zinatarajiwa kupandishwa mwezi wa saba kutoka shilingi elfu moja hadi shilingi elfu tano kwa mtu mkubwa na kutoka mia tano hadi elfu mbili kwa mtoto'' alisema afisa huyo.
Kutoka kulia mkuu wa mkoa wa iringa christine ishengoma, afisa utalii tanapa kanda ya kusini risala kabongo, mkuu wa wilaya kilolo geraid kuninita, na afisa kwa nyuma.
 

Katika ukanda wa kusini Zaidi ya vivutio 78 vimekwisha tambuliwa hadi kufikia 2012, vikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo inaongoza kwa ukubwa Afrika Mashariki, Makumbusho ya Chifu Mkwawa yaliyopo Kalenga, Zama za Mawe za Kale za Isimila  mapango na misitu ya nyumba nitu, mwamba wenye ramani ya afrika wenye ukubwa wa hekari  saba, mpanga kipengele, hifadhi ya Kituro na Mdandu ambako kunapatikana boma la wajerumani na mahakama ya mwanzo iliyojengwa na wajerumani pamoja na mti mkubwa wa asili wa Mlizombe, safu ya milima ya Livingstone, misitu ya miyombo fukwe za ziwa Nyasa, na vingine vingi. 


Itakumbukwa kwamba Mkoa wa Iringa ulitangazwa na serikali kuwa kutovu cha kuendeleza utalii kwa Ukanda wa kusini mwaka 2009.


0 comments:

Post a Comment