MECHI YA MGAMBO, YANGA YAINGIZA MIL 24/-
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mgambo Shooting na Yanga iliyochezwa
jana (Aprili 17 mwaka huu) Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga imeingiza
sh. 24,865,000 kutokana na watazamaji 4,386.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 162 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya
bao 1-1 vilikuwa sh. 10,000 kwa jukwaa kuu na sh. 5,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 5,547,337.50 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 3,792,966.10.
Asilimia
15 ya uwanja sh. 2,820,680.08, msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna
wa mechi sh. 90,000, waamuzi sh. 270,000, maandalizi ya uwanja sh.
100,000 na tiketi sh. 1,587,500.
Mgawo
mwingine ni gharama za mechi sh. 1,692,408.05, Kamati ya Ligi sh.
1,692,408.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 846,204.05
na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) sh. 658,158.69.
MAKOCHA AZAM, FAR RABAT KUTETA
Makocha
wa timu za Azam, Stewart John Hall na AS FAR Rabat ya Morocco,
Abderazzak Khairi watakutana na waandishi wa habari kesho (Aprili 19
mwaka huu) kuzungumzia mechi yao itakayofanyika Jumamosi, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Mkutano
huo ambao pia utawahusisha manahodha wa timu hizo mbili utafanyika saa 5
kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Barabara ya Uhuru na
Shaurimoyo.
Timu
hizo zitakutana katika mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe
la Shirikisho itakayoanza saa 10 kamili jioni. Mechi ya marudiano
itachezwa nchini Morocco wiki mbili baadaye.
JKT RUVU, YANGA KUUMANA JUMAPILI
Yanga
ambayo inafukuzia kwa karibu taji la Ligi Kuu ya Vodacom itapambana na
JKT Ruvu katika mechi pekee ya ligi hiyo wikiendi hii itakayofanyika
Jumapili (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali
ya mechi hiyo, nyingine zitakazochezwa mwezi huu ni kati ya African
Lyon na JKT Ruvu itakayofanyika Aprili 24 kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar
es Salaam wakati Aprili 25 ni kati ya Ruvu Shooting na Simba kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nayo
Coastal Union itaikaribisha Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga katika mechi itakayochezwa Aprili 27. Uwanja wa Taifa utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya Simba na Polisi Morogoro itakayofanyika Aprili
28.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment